Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumzia umuhimu wa matumizi ya Nishati safi kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi [Picha na Paul Mathias] |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwa ifikapo mwaka wa 2034 wananchi wa Mkoa wa Katavi zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa Mkoa wa Katavi watakuwa wanatumia nishatisafi ukiwa ni utekelezaji wa maelelezo ya mwongozo ulitolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Katavi wakipatiwa Elimu kuhusu matumizi ya Majiko banifu yanayomia nishati mbadala kwaajili ya kupikia Majumbani[Picha na Paul Mathias]
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwa ifikapo mwaka wa 2034 wananchi wa Mkoa wa Katavi zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa Mkoa wa Katavi watakuwa wanatumia nishati safi ukiwa ni utekelezaji wa maelelezo ya mwongozo ulitolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Hayo ameyasema wakati alipokuwa akiongea na wandishi wa Habari Ofisini wakati alipokuwa akielezea mikakati mbalimbali iliyowekwa na Mkoa wa Katavi katika kuhakikisha wanafikia lengo hilo .
Mrindoko amesema hivi karibuni Rais Dk Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo na mwongozo kuhusiana na mkakati wa Kitaifa wa nishati safi na katika mkakati huo Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekusudia ifikapo mwaka 2034 inatakiwa zaidi ya asimia 80 ya wananchi wawe wameanza kutumia nishati safi katika kupika na kwenye matumizi mengine yanayotumia nishati .
Wadau mbalimbali wanaouza Majiko yanayotumia Nishati Mbadala wakiendelea kutoa Elimu kwa wananchi Kuhusu matumizi ya Majiko hayo .Picha na Paul Mathias] |
''Mkoa wa Katavi umeanza kufanyia kazi mkakati huu katika Wilaya zote za Mkoa wa Katavi za kuhakikisha ifika mwaka huo wanafikia lengo hilo la wananchi kuwa wanatumia nishati safi ambayo ni gesi ,umeme na majiko banifu ya aina mbalimbali yanayotumia nishati kidogo''-RC Mrindoko
Mrindoko amesema wameanza kutoa elimu kwa Wanananchi katika matumizi ya kutumia nishati kwa kuandaa kongamano la Matumizi ya Nishati Safi kuanzia Tarehe 11/6/2024 hadi Tarehe 13 kongamano ambalo linajulikana kama MWANAMKE NA NISHATI SAFI linalofanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Mpanda Sociall Hall Mpanda Mjini.
Amefafanua kuwa na kwa kiasi kikubwa kwa zaidi ya asilimia 95 litahusisha wanawake na wameamua kutoa nafasi kubwa kwa wanawake kwa kuwa watumiaji wa kwanza wa nishati isiyo safi ni wanawake wanapokuwa wanapika na kuandaa chakula na mambo mengine ndani ya familia .
Amesema faida moja wapo ya kutumia nishati safi kuzuia ukataji miti kwa ajiri ya kutafuta kuni na mkaa kwa ajiri ya kupata nishati ya kupikia.
Mkuu huyo wa Mkoa amewaomba wananchi wa Mkoa wa Kataji na Mikoa ya jirani wafike kuweza kujionea maonyesho hayo na siku ya kilele kutakuwa na mafunzo na maada mbalimbali ambazo zinahusiana na namna bora ya mwanmke kutumia nishati safi ili kutunza mazingira.