WASIO FAHAMIKA WAVUNJA SANAMU YA BIKIRA MARIA PAROKIANI KAREMA. .


Na  Walter  Mguluchuma .
Katavi .
 Katika  hali  isiyotalajiwa  na iliyowashitua  waumini wa    Kanisa  dhehebu  la  Romani  Cathoic (RC)wa  parokia ya Karema na Jimbo la  Mpanda  watu wasio fahamika wamevunja   sanamu ya  Bikilamaria (Golotha) kwenye  Kanisa  la  Parukia ya Karema  na kuivunja mikono  masiko  na  kubeba sehemu yote  poa  na kuondoka nayo .
.
           
Kanisa katoliki Parokia ya Karema jimbo la Mpanda

 Tukio  hilo  ambalo  limevuta  hisia za waumini wa  Parokia hiyo  ya  Jimbo   Katoliki   la Mpanda na watu wengine wa  Mkoa wa Katavi limetokea usiku wa kuamkia tarehe 9 june  parokiani hapo .
.
 Katekisita  Audifax Kauzeni  wa  Parokia  hiyo ambae aliachiwa jukum la kuendesha ibada Parokini  hapo kufatia  Paroko na  msaidizi wa parokia hiyo kuwa safarini  amesema taarifa za kuvunjwa kwa  sanamu  hiyo aliipata   baada ya kuwa wametoka  kwenye ibada ya misa ya juma pili .

Amesema  kuwa siku hiyo ya juma pili  alifika  parokiani hapo  na kuendesha  ibada ya misa ya juma pili  parokiani hapo na mara baada ya kumaliza ibada yeye  na waumini wengine walirudi nyumbani  huku wakiwa hawajuwi kama kuna uharibifu wowote ambao umetokea .

Katekisita Kauzeni  ameeleza  wakati akiwa  nyumbani kwake  anasubiria  kula  mlo wa  mchana alipokea simu kutoka  muumini  mmoja wa Kanisa hilo  alimwambia kuwa  Golotho  la     sanamu  ya  Bikila  Maria la  Parokiani limevunjwa na kuharibiwa na watu wasio fahamika .

Amesema  baada ya  kupokea taarifa hiyo alifika kwa haraka parokiani na aliweza kukuta   Golotho  la  Bikila  Maria likiwa limevunjwa  mikono yoye  miwili na sehemu ya kidevu  huku sehemu ya pua  ikivunjwa na kubebwa  na watu hao ambao  hawajafahamika .

Katekisita  Kauzeni  amesema  wanashindwa kuelewa  lengo la watu  hao kufika  kanisani  hapo  na   kuvunja  sanamu hiyo  na kisha  kuondoka na sehemu ya pua  kama watu hao walikuwa wanadhani  sanamu hiyo imetengenezwa na  vitu vya  thamani madini au    ni kutokana na imani zao za kishirikina .


Paroko wa Parokia ya Karema   Padri  Nicodemo   Kiyumana akizungumza na wandishi wa  Habari hii  akiwa   safarini      Nchini  Kenya amesema  amepokea  taarifahiyo na   amesikitishwa sana na tukio hilo  ambalo  linataka  kuingilia imani za waumini wa Kanisa hilo

Padri Kiyumana ameliomba Jeshi la polisi mkoa wakatavi kufanya jitihada la kuwakamata watu hao walio husika kufanya tukio hilo kwenye Parokia yake.
 .
Parokia ya Karema  inahistoria kubwa ya  Kanisa  Katoliki  hapa   nchini kwani ndio moja ya makanisa  ya     mwanzo hapa  nchini lilianzishwa mwanzoni mwa  mwaka 1880 na  likuwa litumiwa na waumini wa kutoka  nje ya nchi na majimbo ya  Kanisa hilo kwa ajiri ya kufanyia hija mbalimbali

    mwisho  

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages