Mkuu wa Mkoa wa Katavi mwanamvua Mrindoko amewataka wananchi
kuzingatia matumizi ya nishati safi yakupikia na kuachana na uharibifu wa mazingira unao tokana
na ukataji miti hovyo kwaajili ya kuni
na mkaa ili kuimarisha biashara ya hewa ukaa inayo tokana na misitu.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa kongamano la nishati safi
rililo fanyika katika ukumbi wa manispaa yam panda mkoani hapa ambapo amesema
kuwa kuwepo kwa matumizi bora ya nishati safi kwa kila mwananchi kutaenda
kuondoa adha ya uharibifu wa mazingira ambayo mara kadhaa imekuwa ikitokana na ukataji
miti hovyo kwa ajili ya matumizi ya kupikia
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza na wananchi katika kilele cha kongamano la nishati safi
Mrindoko ameeleza kuwa kuwepo kwa matumizi bora ya nishati
safi kutazidi kuimarisha biashara ya hewa ukaa ambayo katika mkoa wakatavi
imekuwa ikifanyika katika wilaya ya Tanganyika .
Amewataka wakuu wawilaya kuhakikisha wanasimamia utoaji wa
elimu juu ya matumizi ya nishati safi
kwa wananchi na kuwasogezea huduma hiyo katika jamii ili kudhibiti
kikamilifu changamoto ya uharibifu wa mazingira ikiwa ni sehemu ya malengo ya
Rais wa jamhuri wa jamhuri ya muungano wa Tanzania samia suluh hassan.
Mrindoko ameshiriki katika ugawaji wa gesi kwa baadhi ya
wananchi ikiwa nisehemu ya hamasa ya matumizi ya nishati safi katika jamii.
Amezidi kubainisha kuwa matumizi ya nishati chafu kwa maana
ya kuni na mkaa yanachangia kuondoa uoto wa asili ,madiliko ya
tabia ya nchi hivyo kuongeza changamoto ya upatikanaji wa nvua zisizo tarajiwa sambamba
na mafuriko kuongezeka katika sehemu mbalimbali.
Pia ametoa ufafanuzi kuwa
kuendelea kuwepo kwa matumizi ya nishati chafu kutachangia kukosekana
kwa mazao ya chakula kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayo changiwa na
ukataji wa misitu hovyo na wananchi watakuwa na hali ngumu ya ukosefu wa
chakula ikiwa wataendelea na uharibifu wa mazingira
Amesema kuwepo kwa matumizi ya nishati safi kutadumisha afya
za wananchi kwani wengi wao wamekuwa wakipata sumu inayo tokana na matumizi ya
nishati chafu kama vile kuni na mkaa.
Baadhi ya wananchi walio hudhuria kongamano hilo wamekili
kuwepo kwa matumizi makubwa ya nishati chafu nakueleza kuwa wanaenda kuimarisha
matumizi ya nishati safi ikiwa nisehemu ya utunzaji wa mazingira huku wakieleza
lengo lao kubwa nikuona biashara ya hewa
ukaa inazidi kukuwa katika vijiji mbalimbali mkoani hapa.
Mwisho