Na Paul Mathias-Katavi
Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limeanza kufanya uchunguzi wa tukio la mkazi mmoja wa wa Dar es salamu Ediger Edison Mwakalebela Miaka 27 baada ya kutekwa tangu 23/6/2024 na kisha kuokotwa akiwa na majeraha Mkoa wa Katavi katika pori la hifadhi ya taifa ya Katavi 26/6/2024.
Ediger Edson Mwakalebela Mkazi wa Mbezi kwa Msuguri anaedaiwa kutekwa siku chache zilizopita na kuokotwa katika Pori la hifadhi ya Taifa ya Katavi. |
Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limeanza kufanya uchunguzi wa tukio la mkazi mmoja wa wa Dar es salamu Ediger Edison Mwakalebela Miaka 27 baada ya kutekwa tangu 23/6/2024 na kisha kuokotwa akiwa na majeraha Mkoa wa Katavi katika pori la hifadhi ya taifa ya Katavi 26/6/2024.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mwakalebela
ameokotwa na wananchi wanaotokea Mpimbwe kuja Mpanda mnamo majira ya asubuhi ya
26/6/2024 akiwa na majeraha kichwani huku watekaji hao kutochukua kitu
chochote.
’Wananchi ambao wanatoka Mpibwe kwenda kuja Mpanda walimuona na kutupatia taarifa kwahiyo tukaenda pale tukamkuta anaelezea kwamba yeye alikuwa akitokea kwa rafiki yake akielekea nyumbani kwake Mbezi----Kaster
Ngonyani ameeleza kuwa kwa sasa mtu huyo anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya halmashauri ya Wilaya ya Mpibwe huku jeshi hilo likisubiria ripoti ya Daktari Juu ya tukio hilo.
Habari ya kutekwa kwa mfanyabiashara huyo zimeanza kuenea kwa kasi katika mitandao mbalimbali ya kijamii mapema leo.