Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akimkabidhi shilingi laki tano mmoja ya askari waliopatiwa tuzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura |
Na Paul Mathis-Katavi
Jeshi la
polisi Mkoa wa Katavi limeobwa kuendelea kuimalisha ulinzi na usalama kwa
wanananchi katika kukabiliana na matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo mauji na
vitendo vya uhalifu.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua mrindoko akitoa neno kwenye hafla ya utoaji wa vyeti kwa baadhi ya askari mkoa wa Katavi waliopatiwa tuzo na IGP
Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limeobwa kuendelea kuimalisha ulinzi na usalama kwa wanananchi katika kukabiliana na matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo mauji na vitendo vya uhalifu.
Wito huo
umetolewa na mkuu wa Mkoa wa Katavi mwanamvua Mrindoko wakati akikabidhi tuzo
kwa askari Saba wa mkoa wa Katavi zilizotolewa na IGP wa Jeshi la Polisi Nchini
Camillus Wambura kwa utendaji wao mzuri wa kazi.
Mrindoko
amesema kuwa mkoa wa katavi umekuwa ukikubwa na baadhi ya matukio ya uvunjifu
wa amani ikiwemo mauaji na kulipiza kisasi jambo ambalo siyo zuri kwa jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko [katikati] akiwa katika picha ya pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi,SACPKaster Ngonyani na baadhi ya maafisa wa polisi waliopatiwa tuzo hizo |
Ameliomba
jeshi hilo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya kujichulia
sharia mkononi pamoja na kulipizana kisasi.
Katika hatua
nyingine amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini Camillus Wambura kwa
kutambua mchango wa askari Saba kwa mkoa wa Katavi kwa kuwatunuku vyeti na
fedha shilingi laki tano kila mmoja.
‘’Tumeshiriki
kuwatunuku nyeti askari hawa saba na fedha shilingi laki tano kila askari
katika zoezi hili tunampongeza mkuu wetu wa Jeshi la polisi IGP Wambura kwa
kutoa tuzo hizi kwa askari hawa --- Kaster.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani akitoa neno la shukurani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillus Wambura kwa kutoa tuzo kwa Askari Saba Mkoa wa Katavi |
Nao baadhi ya askari waliopatiwa tuzo hizo wamemshuru Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini Camilius Wambura kwa kuwapatia tuzo hizo na kuahidi kufanya kazi kwa bidi kwa kuwatumikia wananachi na jeshi la polisi kwa ujumla.