Katavi .
Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira (RUWASA ) Mkoa wa Katavi wamepanga kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 wananchi asilimia 85 wanaoishi vijijini katika Mkoa wa Katavi wawe wamefikiwa na maji safi na salama .
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Ruwasa wa Mkoa wa Katavi Mwandisi Peter Ngunula katika kikao cha wadau wa maji wa Wilaya ya Tanganyika kilicho fanyika katika ukumbi wa Katavi Resort ha wadau mbambali wa maji wakiwepo na wajumbe wa Bodi ya watowa huduma ya maji ngazi ya jamii.
Piter Ngunula meneja Ruwasa Mkoa wakatavi akizungumza na wadau wa maji wawilaya ya Tanganyika katika ukumbi wa Katavi Resort uliopo katika Manispaa ya Mpanda .
Amesema ilikufikia mwaka 2025 [RUWASA ]katika Mkoa wa Katavi watakuwa wamekwisha weka malengo ya kuhakikisha ifikapo mwakani asilimia 85 ya wananchi wanaoishi vijijini watakuwa wanapata maji safi na salama.
Amewataka wadau wa maji wa Halmashauri ya Tanganyika na Wilaya nyingine za Mkoa huu kushirikiana na bodi za watoa huduma ya maji ngazi ya jamii kutoa huduma nzuri ya maji kwa wananchi.
Katika kuhakikisha wanafikia malengo hayo Ruwasa Mkoa wa Katavi wamepokea fedha kwa ajiri ya uchimbaji wa visima 25 vya maji safi na salama ambapo kila jimbo la uchanguzi visima vitano na kwa nchi nzima vitashimbwa visima 900.
Wadau mbalimbali wa maji wawilaya ya Tanganyika wakiwa katika kikao cha kujadili mambo mbalimbali ya upatikanaji wa huduma ya maji kilicho fanyika katika ukumbi wa Katavi Resort kilicho andaliwa na RUWASA Wilaya ya Tanganyika.
Nae Saimoni Kajange Mratibu wa vyombo vya utumiaji huduma ya maji ngazi ya Jamii wa Wilaya ya Tanganyika amesema hadi sasa huduma ya maji kwa wananchi wa Wilaya hiyo wanaopata maji safi na salama imefikia asilimia 78 ambapo Wilaya hiyo ina Kata 16 na vijiji 55.
Hivyo kutokana na asilimia hizo walizofikia kwa sasa Ruwasa Wilaya ya Tanganyika wameweza kuwapunguzia kwa kiasi kikubwa wananchi umbali wa kwenda kutafuta huduma ya maji .
Amefafanua kuwa katika kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inasimamiwa ipasavyo hadi sasa wanajumla ya vyombo sita ambavyo vinasimamia huduma ya utumiaji maji kwenye ngazi ya jamii kwenye maene ya wilaya hiyo .
Ametaja moja ya majukumu ya vyombo hivyo ni kuhakikisha wanaelimisha wananchi kutunza na kulinda vyanzo vya maji ili kuweza kusaidia kwa vizazi vya sasa na vijavyo .
Kwa kuhakikisha hilo linafanyika Ruwasa Tanganyika wameanza kupanda miti kwenye maeneo mbalimbali yaliyokaribu na vyanzo vya maji na kwenye maeneo mengine .
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Busweru akizungumza kwa kina na wadau wa maji wa wilaya ya Tanganyika ambapo ameagiza Taasisi zote zinazo daiwa bili za maji kulipa haraka iwezekanavyo na ameziagiza kamati za ulinzi shirikishi za kuanzia ngazi ya vijiji hadi tarafa kuhakikisha zinalinda miundo mbinu ya maji na miundo mbinu nyingine isi weze kuharibiwa.
Mkuu wawilaya ya Tanganyika Onesmo Busweru ametaja moja ya changamoto kubwa inayovikabili vyombo hivyo vya utoaji huduma kwenye ngazi ya jamii ni ucheleweshaji wa ulipaji wa madeni na hasa kwenye taasisi za Serikali .
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Busweru ameziagiza taasisi zote katika Wilaya hiyo kuakikisha wanalipa madeni hayo wanayo daiwa mapema iwezekavyo .
Amewataka Ruwasa kwenye Wilaya hiyo kuhakikisha swala la maji kwenye miradi yote linakuwa ni kipaumbele na wananchi wapate maji muda wote kwa masaa 24 na sio kumpangia mwananchi muda wa kupata maji .
Amesema Ruwasa wahakikishe wanaweka mifumo ya ulinzi ili miundo mbinu ya maji isiharibiwe na mtu yeyote kwa kuweka ulinzi shirikishi za Vijiji ,Kata na Tarafa kila mmoja awe macho kwenye ulinzi wa miradi ya maji ili kusiwe na kuhujumiwa .
Buswelu amesisitiza kuwa hilo la miundo mbinu lisiwe na kwenye miradi ya maji tuu bali ulinzi huo uwe na kwenye miradi mingine pia.
MWISHO