Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi,SACP Kaster Ngonyani akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya Jeshi hilo katika Mkoa wa Katavi |
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limewakamata watu kumi kwa tuhuma za kujihusisha na matukio tofauti ya mauaji yaliyotokea hivi karibuni katika maeneo tofauti yaliko katika Mkoa wa Katavi .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi,SACP Kaster Ngonyani akionyesha Pikipiki nne zilizokamatwa na Jeshi hilo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina msaidizi Mwandamizi Kaster Ngonyani
amewaambia Wandishi wa Habari wakati akitoa taarifa ya
mafanikio ya jeshi hilo kuwa watuhumiwa hao wote kumi wamekamatwa na jeshi la
polisi kufuatia msako mkali uliofanywa na jeshi hilo .
Ambopo hadi sasa wanaendelea kuwashikilia na mahojiano
yakiwa yanaendelea kufanyika na mara uchunguzi
utakapokuwa umekamilika watafikishwa Mahakamani mara tuu
taratibu za kisheria zitakapokuwa zimekamilika .
Kamanda Ngonyani amesema katika kipindi cha mwezi
mmoja wa Mei mwaka huu wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa
jumla ya 76 wakiwa na vielelezo mbalimbali ambavyo sio
mali yao .