Mkurugenzi wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Stanley Mnozya akizungumnza namna Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inavyoendelea kukuza sekta ta Tumbaku hapa nchini. |
Bodi ya Tumbaku Tanzania imemshukuru Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
Samia Suluhu Hassan kwa kukuza Sekta ya Kilimo hapa
nchini kwa jinsi anavyosimamia kipekee
kuhakikisha sekta hiyo inakuwa yakipekee hapa nchini .
Bodi ya Tumbaku Tanzania imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kukuza Sekta ya Kilimo hapa nchini kwa jinsi anavyosimamia kipekee kuhakikisha sekta hiyo inakuwa yakipekee hapa nchini .
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya
Tumbaku Tanzania Stanley Mnozya wakati aliopuwa
akiongea na wandishi wa Habari wa vyombo
mbalimbali vilivyopo katika Mkoa wa Katavi ,
Amesema kwa hari hiyo wao kama sekta ya
Tumbaku hapa nchini wanaipongeza sana Serikali
ya awamu ya sita kwa kuleta picha na mazingira
tofauti kwenye sekta hiyo hivyo wanamwahidi Rais Dk Samia kuendelea
kufanya kazi kwa bidi na kutumia furusa kwa ajiri ya maendeleo ya
Watanzania
Wakulima wa Tumbaku Amcos ya Filimule wakitembelea shamba la ekari tatu la miti waliyopanda kama sehemu ya kumuunga mkoa Rais Dk Samia katika utunzaji wa mazingira. |
Mnozya amesema ongezeko hili inaonyesha jinsi
ambavyo Serikali ilivyofanya kazi kubwa chini kwa kuleta
mazingira mazuri ya kibiashara na aekta ya tumbaku sasa ipo
juu aliyefanya hivyo Rais apewe maua yake
kwani sekta ya hiyo wametendewa haki na wakulima wanafaidika sana .
Amesema katika msimu huu na msimu
uliopita bado shida ya dola duniani ni kubwa hakuna dola
kunabaadhi ya nchi wanaangaika na msimu uliopita wakulima
wetu walishindwa kulipwa kwa wakati lakini Rais Samia kwa
kupitia Waziri wake wameweka utaratibu wa kuhakikisha wakulima wanalipwa
kwa wakati msimu huu na mpaka Amcos zote nchini zimelipwa
fwdha zao zote .
Amesema Waziri wakilimo Hussein Bashe amekuwa
akifanya kazi kubwa usiku na mchana kwa
kuisimamia vizuri Sekta ya Tumbaku na kwa hayo
hayo mabadiliko huwezi kuacha
kumsema mchango wake mkubwa aliutowa Hussen
Bashe ,
Aidha amemskuru Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kwa kuendelea kufanya maboresho makubwa katika sekta ya Kilimo haswa kwa upande wa zao la Tumbaku ambalo limekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi kwa Taifa.
Hivyo baada ya matatizo ya dola ya msimu uliopita
Rais kupitia Waziri Bashe waliweka
utaratibu wa kuhakikisha dola zinapatikana wakulima walime na
wapate fedha na nijambo ambalo yeye lilikuwa
linampa wasiwasi lakini limetendeka
Agnes Jonh mkulima wa Tumbaku Wilaya ya Mpanda akielezea namna anavyonufaika na kilimo cha zao la Tumbaku. |
Emanuel Kachele wanachama wa Amcos
ya Filimule Wilaya ya Mpanda amemshukuru
Rais Dkt Samia kwa makubwa aliyowafanyia
kwani zao la tumbaku hapo nyuma lilikuwa na
changamoto lakini toka makampuni ya ununuzi
yameingezeka sasa hivi wanapata pesa .
Nae Agripina Cosmas amesema toka ameanza kilimo cha
tumbaku alikuwa haja wahi kupata malipo kwa haraka
kama msimu huu kwani wameweza kulipwa ndani ya mwezi mmoja
toka wauze tumbaku yao.
Kwa upande wake Kassimu Vedelemto amesema kazi kubwa imefanywa na Rais na Waziri wa kilimo kwa kuweza kuwajali wakulima wa tumbaku hadi wadogo na hivyo wao hawatawaangusha katika uzalishaji .
Alisema kila safari inamilima na mabonde lakini kwa kipindi hiki sasa huu muda kwa wakulima safari sasa imefika na kazi hiyo imefanywa na serikali kwa kuleta makanpuni mwaka huu fedha imefika kwa wakati watu wanajenga nyumba na wananunua pikipiki.