Na Walter Mguluchuma
Katavi
Waziri Mkuu msataafu Mizengo Pinda amesema swaala la mmonyoko
wa maadili linatakiwa kuanza kufundishwa
mashuleni kuanzia awali ili kuchangia katika mafunzo wanayokuwa wameyapata toka nyumbani kwa Baba na mama ili mtu aanze kujua kwanini swala la maadili linazungumzwa kwa ukubwa
kiasi hicho.
Wito huu ameutoa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari wa vyombo mbali mbali walioko katika Mkoa wa Katavi walipo mtembelea
kwenye makazi yake katika Kijiji cha Kibaoni Halimashauri ya Mpimbwe wilaya ya
Mlele .
Amesema tusianze kulaumiana kwenye swaala la maadili ila jambo kubwa ni kutambua kuwa mwana umleavyo ndivyo akuavyo samaki mkunje angali akiwa mbichi usingoje akauke kwa hiyo mtu wa kwanza kabisa anae paswa kubeba jukumu la malezi ya mtoto ni Baba na mama hivyo wa najua hilo na wana timiza wajibu wao wa kuwa kuza watoto ili wasije wakaenda kinyume na maadili.
Pinda amebainisha kundi la pili katika malezi ya mtoto ni shule anako pata elimu je walimu swaala la maadili wanafundisha mashuleni ili kuchangia katika mafunzo ya Baba na mama na ndiyo maana watu wanapendekeza swaala la maadili liwe somo katika shule zetu kuanzia awali ili mtu aanze kujua nini hiki kinacho zungumzwa kwa uzito kiasi hiki.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Katikati akiwa na baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Katavi walio hudhuria kusikiliza mazungumzo yake ya maswaala mbalimbali ya kimaendeleo katika Mkoa wa katavi na jamii kwa ujumla .
Jamii yenyewe kwa ujumla inao wajibu wanapokuwa wamemuona
mtoto amefanya jambo kinyume na maadili wasinyamaze watoe taarifa kwa wazazi
lakini hana uhakika kama kweli jamii inatimiza wajibu huo.
Amesema viongozi wa madhehebu ya Dini wana nafasi kubwa sana
kwenye eneo hili kwani mengi yanayo husu mmonyoko wa maadili kwa sababu mengi
ni yale yanayo husu makatazo ambayo yanakinzana na maagizo yanayo patikana
kwenye vitabu vitakatifu .
Kwahiyo kunapaswa kuwa na zamu za viongozi wa Dini kwenda
kutoa mafunzo mashuleni ili kuunganisha yale mafunzo ya Baba na Mama Kanisani
na kwenye jamii nayale ya shuleni.
Amefafanua kuwa utandawazi nao pia umekuwa nichangamoto
kubwa katika kusababisha mmonyoko wa maadili unakuta mtoto wa miaka 14 anataka
kumiliki simu janja ndio maana nchi nyingine watoto wadogo hawaruhusiwi
kumiliki simu janja.
Hivyo nilazima tufikie maadili tuanze kuona na kubadili
mifumo yetu ya namna ya kuwakuza watoto
wetu kwa njia mbalimbali hivyo nilazima wazazi wawe wakali pindi mtu anapo kuwa
amevunja maadili kwamfano unakuta mtu mzima amebaka mtoto wa miaka mi tatu au
mama yake mzazi jambo hilo aliwezi kukaliwa kimya hata kidogo.
Mwisho