Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk,Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wanananchi wa Mkoa wa Katavi baada ya kuwasili Mkoa wa Katavi. |
Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk, Samia suluhu Hassan akipata maelezo ya ujenzi wa mradi wa jengo la abiria uwanja wa Ndege Mpanda |
Rais wa Jumuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amewasili katika Mkoa wa Katavi kuanza ziara ya kikazi ya Siku Nne.
Muda mchache baada ya kuwasili
katika uwanja wa ndege Mpanda Rais Dk Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Jengo
la Abiria uwanja wa ndege wa Mpanda ambalo
limegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.4.
Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa jengo
hilo la abiria uwanja wa ndege Mpanda Mkurugenzi Mkuu wa wa mamlaka ya viwanja
vya Ndege Tanzania Mussa Mbura ameishukuru serikali kwa kuleta fedha kwaajili
ya ujenzi huo.
Jengo jipya la Abiria uwanja wa Ndege Mpanda ambalo limejengwa na serikali kwa shilingi Bilioni 1.4 |
Mbura amesema jengo Hilo jipya la abiria mpaka kukamilika na kuanza kutumika litumia kiasi cha shilingi Billion 1.4 fedha ambazo zinajumuisha mifumo yote ikiwemo mifumo ya CCTV,mifumo ya uzimaji moto,mifumo ya kuchakata taarifa za abiria wanapoingia kwenye uwanja wa ndege, sehemu ya kuegesha magari na mifumo mingine inayohitajika kwenye jengo hilo.
Rais Dk samia Suluhu Hassan anatarajia kuwamgeni Rasmi kwenye Kufunga maadhimisho ya wiki ya jumuiya ya wazazi Kitaifa yatakayo fungwa rasmi 13,Julai 2024 katika uwanja wa CCM Azimio Mpanda Mjini.Pamoja na maadhimisho hayo Rais Dk Samia Suluhu Hassan atatembelea miradi ya maendeleo katika mkoa wa Katavi ikiwemo kituo cha kupozea umeme wa Gridi ya Taifa kutoka Tabora Mpanda katika wilaya ya Mlele pamoja na kutembelea miradi mingine ya maendeleo Mkoa wa Katavi.