MANISPAA YA MPANDA WAVUKA LENGO LA MAKUSANYO YA NDANI 2023/2024.

 








 

MANISPAA YA   MPANDA  WAVUKA LENGO LA MAKUSANYO YA NDANI  2023/2024.

Na  Walter Mguluchuma

     Katavi

Manispaa ya  Mpanda Mkoa wa  Katavi  wamefanikiwa  kuvuka  lengo la  makusanyo ya   mapato ya  ndani kwa  zaidi ya asilimia   100 kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 kutokana  na   jitihada  kubwa  zilifanywa na Manispaa katika  ukusanyaji wa  Mapato ya   ndani .

Hayo  yamesemwa  na  Meya wa Manispaa ya  Mpanda  Haidari  Sumry  wakati wa kikao   cha  Baraza  la   Madiwani wa  Halmashauri  hiyo kilichofanyika  katika ukumbi wa Manispaa ya  Mpanda alipokuwa akiwasilisha taarifa ya  kamati  ya   fedha na   uchumi .

                  


Maya wa Manispaa ya Mpanda Haidari Sumry akielezea Manispaa ya Mpanda ilivyo weza kuvuka lengo la makusanyo ya mapato ya ndani kwa mwaka 2023/2024 kwa kukusanya asilimia 106  

Sumry amelieleza   baraza  hilo kuwa    kwa  msimu wa  fedha wa 2023/ 2024 Manispaa  hiyo  ilipanga  kukusanya  kiasi   cha  Bilioni  3,204,740,000 hata  hivyo wamefamikiwa  kuvuka  lengo na  kukusanya kiasi  cha shilingi Bilioni 3,397,159,301,4.49 ambayo  mapato  hayo  ni   sawa  na  asilimia 106.

Amebainisha  kuwa wameweza  kufanikiwa  kivuka  lengo  hilo  la  ukusanyaji wa  mapato yao  ya  ndani kutokana  na  Manispaa  kufanya  kazi  ya  usanyaji wa  mapato kwa  jitihada kubwa  kwa uaminifu na  kudhibiti  mianya   yote ya  utoroshaji wa  mapato .


Maya wa Manispaa ya Mpanda Haidari Sumry katikati akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli pamoja na Naibu Maya wakati wakiongoza Baraza la Madiwani

Kihusu   miradi ya  Maendeleo  amesema  kwa  kipindi  cha  mwezi  mmoja wa  june   2024 Manispa ya  Mpanda wameweza  kupokea kiasi cha  shilingi  Bilioni  5. 4 kwa  ajiri ya  ujenzi  wa shule     mpya   maalumu ya wavulana  na  shule ya  msingi   mmoja  na  matundu ya vyoo.

 Diwani wa  Kaya ya Majengo  Willy Mbogo  amesema  jitihada  hizo  kubwa za ukusanyaji wa  mapato  ziendelee  ili     kuifanya  Manispaa ya  Mpanda  ifikie kuleta  maendeleo  mahali ambapo imepanga kufika ,

Diwani wa Kata ya Majengo Williy Mbogo akiwapongeza wataalam wa Manispaa ya Mpanda pamoja na Madiwani kwa kuweza kukusanya mapato ya ndani kwa zaidi ya asilimia 100

Pia  alimpongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya  Mpanda  Sofia Kumbuli  na  timu yake ya wataalamu   pamoja na madiwani  kwa  ishirikiano wao ulioweza kufanikisha  kukusanya  mapato kwa asilimia 106.

   ,Mwisho

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages