VIONGOZI WA DINI
WATAKIWA KUWAELIMISHA WAUMI MADHARA YA
RUSHWA WAKATI WA UCHAGUZI.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Taasisi ya Kuzuia
na Kipambana na
Rushwa (TAKUKURU)Mkoa wa Katavi imewataka
viongozi wa madhehebu yote
ya Dini
yalioko katika Mkoa wa
Katavi kuwaelezea waumini
wao kwenye nyumba zao za
ibada madhara ya kuwachagua viongozi wanaotokana na Rushwa katika kipindi
hiki cha kuelekea uchaguzi wa
Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu wa mwakani .
Wito huo umetolewa
na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Faustine
Maijo wakati alipokuwa akifunga
mafunzo ya siku
moja ya kuwajengea uwezo viongozi
wa madhehebu ya Dini
na wajumbe wa kamati
ya amani na malidhiano
juu madhara ya kuwapata viongozi
wanao tokana na
Rushwa .
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Faustine Maijo akiwaeeleza viongozi wa madhehebu ya Dini juu ya umuhimu wa kuwa elimisha waumini wao madhara ya rushwa kipindi cha uchaguzi.
Maijo amesema viogozi wa Dini watumie nafasi
kuwaambia na kuwaelimisha waumuni wao
kwenye nyumba zao za ibada
madhara ya kuwapata viongozi
wanaotokana na Rushwa ambapo wanapaswa watambue wakisha wachagua watarudishaje fedha
zao wanazo wapatia au
vitenge ,kanga ,
chakula na vinywaji wanavyo kuwa wamewapatia .
Kwa maana nafasi ambazo
wanataka kuwapa ni lazima
wataanza kwanza kurudisha fedha
zao kwa
sababu hakuna mtu
yeyote ambae anatowa
fedha zake na asijue zinarudishwaje hivyo wawa elimishe waumini wao wawe
na ujasiri wa kuhoji endapo watawachagua wagombea wanaowapatia na vitu vingine fedha
hizo watazireshaje .
Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ilembo Jimbo katoliki la Mpanda Gaspher Katagwa akitoa mchango juu ya umuhimu wa kuwaelimisha wananchi kama viongozi wa Dini juu ya vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu na umuhimu wa wananchi kuwa na uwelewa wa kuijua katiba ya nchi ili wawe na uelewa wa kujua zaki zao za Msingi.
Mkuu huyo wa Takukuru wa
Mkoa wa Katavi
ameeleza kuwa wakumbuke kuwa
hao viongozi watakao kuwa wamewachagua ndio watakao
simamia miradi yote na
pesa nyingi za
maendeleo kwenye maeneo yao amehoji je hawatashindwa kuwahujumu wananchi
kwa hali
hiyo watafute viongozi wa
hadilifu na wenye hofu ya watakao
simamia rasilimali .
Amewasisitiza
viongozi wa Dini wakemee kwa
nguvu zote watu
wote wanao kiuka maadali ya
serikali ambao wanataka
kujinufaisha kwa manufaa yao binafsi na wasikemee tuu watu ambao wanagombee nafasi za
uongozi tuu bali wakemee maovu yote wanayo yaona .
Maijo amewaomba
viongozi hao wa madhehebu
ya dini
kutoa taarifa wakati wowote
kwenye Taasisi hiyo pindi
wanapokuwa wameona kuna viashiria
vya rushwa ili
Takukuru waweze kuchukua hatua
kwa haraka .
Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ilembo Padri Gaspher Katagwa amesema moja ya sababu inayochangia Rushwa ni kutokana na WaTanzania waliowengi awaijuwi katiba hivyo imekuwa ikisababisha watu kutojua haki zao za msingi .
Amebainisha kuwa viongozi waliopo Serikalini ni waumini
wao je
wao kama viongozi wa
dini wanapata muda wa kukaa nao na kuwaeleza wawe
na dhamira safi
na tabia njema kwa sababu
wapo baadhi ya watu wanaona Rushwa na wizi
ni jambo la kawaida
kitu ambacho sio kweli .
Katibu wa Bakwata
wa Mkoa wa Katavi Omari Mona
kitendo cha kipokea rushwa ni
dhambi na mtu ambae
anapokea Rushwa atambue kuwa
anajiretea matatizo kwenye nyumba
yake na kwenye familia yake kwani kile
ulichokipoa kutokana na riushwa
utakapo kitumia huenda kikakuletea matatizo.
Amesema swala la rushwa wamekuwa wanalisema sana
na wataendelea kulisema kwani
wao kama viongozi wa dini wamepewa wajibu wa kuwaeleza waumini wao
kuyakataa mabaya hivyo wao huo ni wajibu wao .
WISHO