RAIS WA ZANZIBAR KUZINDUA WIKI YA WAZAZI MKOA WA KATAVI.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza na waandishi wa Habari wa Mkoa ofisini kwake 

 Na Paul Mathias-Katavi

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa wiki ya jumuiya ya wazazi ccm ambayo kitaifa itafanyika mkoa wa  Katavi.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa wiki ya jumuiya ya wazazi ccm ambayo kitaifa itafanyika mkoa wa  Katavi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko amesema Rais mwinyi atawasili mkoani katavi Julai 8 mwaka huu majira ya asubuhi katika Uwanja wa Ndenge Mpanda nakisha kuelekea katika wilaya ya Mlele ambapo atazindua wiki ya Jumuiya ya wazazi katika shule ya Msingi Inyonga iliyopo katika wilaya hiyo.

Mrindoko amesema Rais mwinyi atafanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ya chama na serikali iliyotekelezwa katika wilaya ya Mlele na Mkoa wa Katavi kwa ujumla.

Aidha Mrindoko amesema baada ya ufunguzi wa wiki ya wazazi kutakuwepo na mfululizo wa viongozi mbalimbali wa kitaifa wa chama na serikali watafika mkoani katavi na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na kutembelea miradi ya maendeleo .

Viongozi hao ni naibu waziri mkuu Dotto Biteko,Makamu mwenyekiti wa CCM  Bara Abdulrahman Kinana na Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufungwa na Rais Dkt.samai Suluhu Hassan Julai 13 mwaka huu katika uwanja wa CCM azimio  Manispaa ya Mpanda Mkoani katavi.

"Tunayo heshima kubwa ya kuwaeleza wananchi wa mkoa wa katavi na mikoa jirani kuwa tunatarajia kupokea ugeni mkubwa wa viongozi mbalimbali wa chama na serikali katika mkoa wetu Kwa ajili ya Maadhimisho ya wiki ya wazazi ambayo kitaifa itafanyika hapa katavi’’-Mrindoko

Taarifa hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi imeeleza kuwa Rais Dk Hussein Mwinyi pamoja na kuzindua Maadhimisho hayo ya Wiki ya Jumuiya ya wazazi atapata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali ya chama na Serikali iliyotekelezwa na serikali Katika Wilaya ya Mlele.

Tunawakaribisha wananchi wote kujitokeza Kwa wingi maeneo yote ambayo rais mwinyi atatembelea kuonesha shamrashamra na hamasa kuonesha upendo Kwa kiongozi wetu"-Mrindoko.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages