Mjumbe wa tume huru ya uchaguzi ambae pia ni Jaji wa Mahakama Kuu Mh Asina Omari akifungua Mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa katavi uliofanyika leo tarehe 8 July ,2024 |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Viongozi wa dini ,Mila ,Asasi za kiraia na makundi ya vijana na walemavu Mkoani Katavi wametakiwa kuhamasisha wananchi kupitia majukwaa yao ya kisiasa ,kiimani,Kijamii na Kitamaduni wajitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa kila mwananchi mwenye sifa.
Wadau mbalimbali wa uchaguzi wakiwa katika kikao wakisikiliza kwa makini maada zilizowasilishwa kuhusu uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura. |
Wito huo umetolewa na Jaji wa
mahakama kuu Asina Omari ambae ni Mjumbe wa tume ya uchaguzi wakati wa mkutano
wa wadau wa uchaguzi wenye lengo la
uboreshaji wa daftari la kudumu la
wapiga kura uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Amesema katika utekelezaji wa
jukumu hilo Tume imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kutosha
kuhusu uboreshaji huo njia mbalimbali za
kutoa elimu ya mpiga kura zitatumika kuhakikisha wadau wote wanapata furusa ya
kuelimika na kuelewa mambo yote ya msingi kuhusu oboreshaji wa daftari ili
waweze kujitokeza kwa wingi.
Givness Aswile Mkurugenzi idara ya habari na elimu kwa mpiga kura wa Tume Huru ya Uchaguzi akielezea INEC ilivyojipanga katika kuborsha daftari la kudumu la Mpiga kura. |
Asina amebainisha kuwa Tume imekuwa
na utaratibu wa mara kwa,mara kuwashirikisha
wadau mbalimbali katika kutekelezaji wa majukumu yake na ndio maana Tume hiyo
ipo Mkoani Katavi kwa lengo la kuwashirikisha wadau mbalimbali.
amesema kikao hicho kitakuwa na
manufaa makubwa katika kutekeleza zoezi lililo mbele hivyo anamruhusu kila
mwananchi mwenye sifa za kuandikishwa kuwa mpiga kura mwenye sifa na kuboresha
sifa zake.
Baadhi ya Wadau wa uchaguzi katika mkoa wa Katavi wakiwa katika kikao hicho |
Amefafanua kuwa Mkoa wa Katavi umekuwa ni miongoni mwa Mkoa wa mwanzo kupata furusa ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura uboreshwaji huo unatarajiwa kuzinduliwa tareh 20 Julai Mkoani Kigoma na mgeni rasimi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Amesema kama mnavyo fahamu Nchi yetu ipo katika maandalizi ya uchaguzi wa 2025 katika maandalizi hayo Tume echini ya ibara ya 74(6) ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imepewa mamlaka ya kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwa na jukumu la kusimamia na kuratibu uandikishaji wa piga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Raisi, wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Madiwani wa Tanzania bara.
Tume imeweka utaratibu kwa watu wenye ulemavu, wazee na wagonjwa kupata huduma bila kupanga foleni na kila chama cha siasa kitaruhusiwa kuweka wakala mmoja kwa kila kituo cha kupigia kura alisema Asina Omari.
Nae Shekhe mkuu wa Mkoa wa Katavi
Mashaka Kakulukulu ameishukuru tume ya
uchaguzi kwa kuwapatia uelewa wa pamoja
kwani wengine hukosa nafasi ya kuto kupiga kura kutokana na kutokuwa na uelewa
wa kutambua umuhimu wa kupiga kura kwa elimu walio pata watahakikisha wanahamasisha
waumini wao waone umuhimu wa kupiga kura
ili waweze kuwachagua viongozi watakao kuwa wanawataka wao.
Ameeleza kuwa ni mafunzo yatakayo wezesha kuweza kwenda kueleza vizuri kwa waumini wao kile ambacho kitakacho fanyika katika uboreshwaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura.