Rais wa Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan |
George Mwigulu na Paul Mathias, Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dk Samia Suluhu Hassan anatarajia kufunga kilele cha wiki ya Jumuiya ya Wazazi wa chama hicho pamoja na kufanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya wijio wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan Mkoani Katavi.
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko akitoa taarifa hiyo Julai 10, 2024
ofisini kwake mbele ya Wanahabari amesema kuwa Rais atafika mkoani humo Julai
12, 2024 na kufanya ziara ya kikazi hadi Julai 15, 2024.
Mrindoko
amesema kuwa Julai 12, 2024 Rais Dk Samia licha ya kuwasili katika uwanja wa
ndege Mpanda atatembelea jingo la abiria uwanjani hapo.
Ameeleza
kuwa akiwa Mkoani Katavi atakuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha wiki ya Jumuiya
ya Wazazi kitaifa ambayo itafungwa Julai 13, 2024 rasmi katika uwanja wa CCM
Azimio manispaa ya Mpanda.
“Kwenye
kilele cha maanzimisho ya wiki ya wazazi Rais Dk Samia Suluhu Hassan
atazungumza na wananchi wa mkoa wa Katavi kupitia mkutano wa hadhara” Amesema
Mrindoko.
Vilevile
atakagua kituo cha kupozea umeme wilaya ya Mlele ambapo umeme wa gridi ya taifa
kutoka Mkoa wa Tabora utapokelewa na kupozwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Julai
14, 2024 ameeleza kuwa Rais atafungua jengo jipya la ofisi ya Kamanda wa Jeshi
la Polisi Mkoa wa Katavi na kufanya uzinduzi wa maghala ya kutunzia mazao
katika eneo la Mpanda Hotel yanayo milikiwa na taasisi ya serikali ya NFRA.
Aidha
Julai 15, 2024 anatarajiwa kutembelea ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Katavi ambapo atahitimisha kusalimiana na wananchi wa kijiji cha Kibaoni
halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe.
Mkuu
wa Mkoa huyo amewaomba wanananchi wa Mkoa wa Katavi kundelea kuimarisha amani
na utulivu huku akiwaomba kujitokeza kwa wingi.