DC MPANDA ATANGAZA VITA KWA WATAKAO BAINIKA KUFANYA UKATILI
WA KIJINSIA KWA WATOTO KATIAKA JAMII.
Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ametangaza vita ya
kuwachukulia hatua kali kwa mtu yeyote
ambae atakae bainika kufanya vitendo vya ukatili wakijinsia kwa watoto wadogo
na kwenye jamii wanayo ishi.
Mkuu wawilaya ya Mpanda Jamila yusuph akizungumza na wana nchi wa eneo la uchimbaji wa Madini ya Dhahabu rililopo katika kijiji cha Dilifu kilichopo katika Manispaa ya Mpanda juu ya ukatili wa kijinsia wanao fanyiwa watoto wakiume na wakike kwenye jamii
Onyo hilo amelitoa alipokuwa akiwahutubia wananchi wa eneo
la uchimbaji wa Madini ya Dhahabu Katika kijiji cha Dilifu kilichopo katika
Manispaa ya Mpanda kufuatia kuwepo kwa baadhi ya matukio ya ukatili wa kijinsia
kwenye eneo hilo la uchimbaji wa Madini.
Amesema katika eneo hilo kumekuwepo na matukio ya kubakwa na
kulawitiwa kwa watoto wa kiume watoto wa kiume sasa hivi wanapitia mazingira
magumu sana hivyo nilazima kuweka nguvu kubwa sana ya kuwalinda watoto wa kiume
ili wasifanyiwe vitendo vya ukatili.
Dc Jamila amesisitiza kuwa Serikali ya Wilaya ya Mpanda
haiku tayari kuona vitendo hivyo vinatokea na watakao jalibu kufanya ukatili
huo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwasababu nao watoto wa kiume wanao umuhimu mkubwa kwenye jamii yetu.
Amebainisha kuwa changamoto hizo ni nyingi sana hata kwa
watoto wa kike kutokana na tabia ya kuwalazamajumbani watoto wadogo na ndungu wanao kuwa wamefikia
kwa wazazi wao kutokana na huwezo mdogo wa nyumba kuwa na vyumba vi chache na
kupelekea watoto wadogo kulazwa chumba kimoja na watu wazima.
Ameeleza kuwa kutokana na mchanganyiko huo wa kuwalaza
watoto kwenye chumba kimoja kumekuwa kukisababisha mtu mkubwa kumbaka mdogo ama
kaka kumlawiti mdogo wake.
Amewasisitiza wakina mama kuwa na utaratibu wa kutumia muda
wao kuwakagua watoto wao wakike na wakiume ili kuweza kubaini kama wamefanyiwa
vitendo vya ukatili wa kijinsia kwani wameisha baini kwenye baadhi ya maeneo
watoto wanafanyiwa vitendo vya ukatili pasipo wazazi wao kujua kutokana na
wazazi kutokuwa na muda wa kuzungumza na watoto wao.
Amewataka wazazi wa kiume nao kukaa na kuzungumza na watoto
wao kwani swaala la ulinzi na usalama kwa mtoto si la serikali peke yake lazima
ulinzi uanzie nyumbani kwahiyo watoto wa kiume wana mazingira magumu kama
ilivyo kwa watoto wa kike na tusipo walinda watoto wetu sasa hivi tuta
tengeneza kizazi cha ajabu.
Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Mpanda Agines Bulaganya
amesema watoto wengi wanabakwqa na kulawitiwa kwa sababu wanakuwa hawana sehebu
ya kusemea wazazi wawe marafiki wa watoto kwa kuwanao kalibu kwa sababu mzazi
ananafasi ya kumfanya mtoto akuwe kwenye maadili mema.