Wananchi wa Mkoa
wa Katavi wanaondokana na usumbufu waliokuwa wakiupata kusafiri
kwenda umbali mrefu kwenda nje ya Mkoa wa Katavi kwenda
kupatiwa matibabu ya salatani ya shingo ya kizazi
baada ya kupatiwa mashine ya upasuaji na
kupima Saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawak na Taasisi ya
WALTER REED yenye thamani ya zaidi ya shilingi
Milioni 62.
Wananchi wa Mkoa wa Katavi wanaondokana na usumbufu waliokuwa wakiupata kusafiri kwenda umbali mrefu kwenda nje ya Mkoa wa Katavi kwenda kupatiwa matibabu ya salatani ya shingo ya kizazi baada ya kupatiwa mashine ya upasuaji na kupima Saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawak na Taasisi ya WALTER REED yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 62.
Msaada huo
umekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua
Mrindoko na Jofrey Ndondole Meneja Mradi wa
(HJFMRJ) katika hafla ya makabidhiano iliofanyika
katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Katavi .
Akizungumnza baada ya
kupokea mashine hiyo iliyotolewa na Taasisi ya Walter Reed Mkuu wa mkoa
wa Katavi Mwanamvua mrindoko amesema mashine hiyo itakuwa mkombozi kwa wanawake
kuepuka kusafiri umbali muda mrefu kufuata huduma hiyo mikoa ya Jirani.
Amebainisha kuwa
huduma za afya katika Mkoa wa Katavi
zimeendelea kuboreshwa siku hadi siku na kuwapunguzia
wananchi adha ya kutembea umbali mrefu kwenda nje
ya Mkoa na kutumia gharama kubwa kwaajiri ya
kwenda kupatiwa huduma hiyo.Meneja mradi wa [HJFMTJ] Jofley Ndondole akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhi Mashine ya uchunguzi wa saratani ya Shingo ya Kizazi
Kwa sasa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambayo ni mpya imekuwa ikiendelea kupata maboresho ya hatua kwa hatua kwa ajiri ya kuimalisha huduma muhimu ya afya kwa ajiri ya wananchi kwani wananchi wanaendelea kupata huduma za kawaida na za kibingwa
Mrindoko
ameeleza kuwa vifaa hivyo ni vifaa
ambavyo vimekuja kufanya kazi kubwa ambayo
ilikuwa haifanyiki hapo awali katika Mkoa wa
Katavi hivyo wahakikishe wanavitunza na kuvitumia kwa
kazi mahususi ambayo imekusudiwa na kutoa
huduma bora kwa akina mama ambao watakuwa wanafika
hospitalini hapo kwa ajiri ya matibabu hayo
ya salatani ya shingo ya kizazi .
Amewataka wanawake
wote wa Mkoa wa Katavi wenye umri wa kuanzia
miaka 21 kufika hospitalini hapo ili waweze kufanyiwa
utafiti wa vipimo ili kuweza kubaini kama
wanatatizo la salatani ya shingo ya kizazi
katika hatua za awali ili waweze kupatiwa
matibabu kwenye hospitali hiyo hiyo ya Mkoa wa
Katavi badala ya kwenda nje ya Mkoa .
Amewasisitiza viongozi wote wa Mkoa huu kuwafahamisha wananchi kuwa sasa wamepata vifaa hivyo kwa ajiri ya matibabu ya awali ya salatani ya shingo ya kizazi na waitumie fursa hiyo vizuri kwa wananchi wote hasa wanawake kwa ajiri ya kupimwa na kupatiwa matibabu .
Kaimu
Mganga Mkuu mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Katavi Dk Frenk Elisha
amesema kuwa tatizo la ugonjwa salatani ya shingo ya kizazi
kwa wanawake katika Mkoa huu lipo kwani
Hositalini hapo kila mwezi huwa wanapokea wagonjwa kati ya 20
hadi 40 na wanaogundulika huwa ni wanawake watatu hadi
saba kwa mwezi .
Uwepo wa
mashine hizo kutasaidia upasuaji utaanza kufanyika hapa
hapa Katavi badala ya wagonjwa kwenda
nje ya Mkoa na utawaokoa sana wanawake wa
Mkoa huu..
Dk Elisha ameishukuru Serikali kwa kuwaza kuwatafutia wadau ambao wamweza kuwaletea mashine hizo ambazo hapa awali hazikuwepo kabisa na pia WALTER RED wamewapatia na friji kwa ajiri ya maabara na mawasiliano simu kwa ajiri ya chumba kimoja kwenda chumba kingine
Meneja wa Mradi
wa (HJFMTJ) Jofrey Ndondole amesema wao kama wadau
wa sekta ya afya wataendelea kuiunga mkono
Serikali katika swala zima la uboreshaji wa afya
hapa nchini .