MBUNGE KAPUFI AWAFUNDA WANACCM KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU.

 MBUNGE KAPUFI AWAFUNDA WANACCM KUELEKEA  UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU.


Na IRENE TEMU 
Katavi

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Mkoani  Katavi,Sebastian Kapufi amewataka Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuitangaza miradi iliyotekelezwa na serikali kupitia Ilani ya CCM kuelekea Uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu 2025.



Kapufi ameyasema hayo katika mkutano wa ndani wa Halmashauri Kuu ya kata Kakese ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake aliyoianza  katika kata ya Mwamkulu Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ya kuzungumza na Viongozi wa Halmashauri kuu za kata 15 zilizopo katika Jimbo lake la Mpanda Mjini 


    Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Sebastiani Kapufi akizungumza katika mkutano wa ndani wa Halimashauri kuu ya Kata ya kakese

Amewataka Viongozi wa CCM na wanachama wake kuyatangaza mazuri yote yaliyotekelezwa na serikali kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi  huku akiwataka kuwachagua viongozi wazuri katika uchaguzi wa serikali  za mitaa watakao kivusha Chama katika uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani mwakan
i.

"niwaombe sana wanaccm wenzangu,katika uchaguzi wa serikali za mitaa,tuwachague wenyeviti wanaofaa kwa kuwabeba na kuwapigani,tuache makundi ambayo yanaanzishwa na sisi wanaccm wenyewe badala yake tukipiganie chama kwa upendo na mshikamano"Mbunge Kapufi



 Baadhi ya wajumbe walio hudhuria katika mkutano huo wakimsikiliza mbunge wakati akizungumza katika mkutano wa ndani wa Halimashauri  kuu ya Kakese



Kapufi amewasisitiza pia wanachama wa CCM kuisemea serikali sambamba na miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa ili iwe chachu ya mafanikio katika chaguzi zijazo.


Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleao katika kata ya Kakese,Mtendaji wa kata hiyo  Noria Bukuku amemwomba Mbunge Kapufi kuendelea kuisemea kata ya Kakese na vitongoji vyake ili baadhi ya miradi iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi ikiwepo maboma ya shule na kituo cha polisi viweze kupatiwa fedha kwa ajili ya umaliziaji.





Nao baadhi ya wanachama wa CCM akiwepo Rose Charles wamemshukuru Mbunge Kapufi kufika katika kata yao na kumwomba aendelea kujitolewa kwa ajili ya maendeleo ya kata na  watu wake kwani amekuwa akiwagusa katika mahitaji na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata hiyo.

MWISHO

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages