Baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Mpanda wanaolalamikia kutolipwa fidia zao ili kupisha mradi wa Maji wa Miji 28. |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Wananchi wapatao kaya zaidi ya 500 wa Mitaa ya Shanwe, Mtemi Beda na Mtaa wa Kigamboni katika Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wametishia kuujumu mradi wa maji wa bwawa la milala unaotekelezwa kwa zaidi ya Shilingi Bilioni 22 kwa madai ya kutolipwa fidia ya maeneo yao kwa muda mrefu wanayoishi na wanayofanyia shughuli za kibinadamu.
Wananchi wapatao kaya zaidi ya 500 wa Mitaa ya Shanwe, Mtemi Beda na Mtaa wa Kigamboni katika Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wametishia kuujumu mradi wa maji wa bwawa la milala unaotekelezwa kwa zaidi ya Shilingi Bilioni 22 kwa madai ya kutolipwa fidia ya maeneo yao kwa muda mrefu wanayoishi na wanayofanyia shughuli za kibinadamu.
Wananchi hao wa mitaa mitatu
hiyo wametowa kauli hiyo walipokuwa wakizungumza na vyombo
mbalimbali vya habari kuhusiana
na kilio chao hicho cha madai ya maeneo yao
wanayoishi na wengine kuhama kwenye maeneo hayo kwa ajiri ya kupisha mradi huo unao simamiwa na mamlaka
ya Maji sahi na usafi wa Mazingira (MUWASA)Manispaa ya Mpanda .
Mradi huo wa Maji wa miji 28
katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda unatekelezwa na Serikali ya Tanzania
kwa ushirikiano wa Serikali ya India ambao hadi kukamilika kwake unatarajia kugharimu
kiasi cha shilingi Bilioni 22.
Mwenyekiti wa wahanga hao Peter Matiyampula
amesema toka mwaka mwaka jana walipofanyiwa tathimini kwa lengo
ya kulipwa fidia yao ya makazi
yao na maeneo wanayofanyia shughuli zao za kilimo lakini
hadi sasa hawajalipwa fidia yao .
Baadhi ya Mabomba ya Maji yakiwa katika eneo la mradi ambao wananchi wanalalamikia kutolipwa fidia zao |
Amesema wapo baadhi ya watu nyumba zao zimeanguka na wamelazimika kwenda kupanga nyumba kwenye maeneo maeneo
mengine kwa kutegemea malipo ya fidia kwenye maeneo hayo.
Jonh Konchela mmmoja wa
wanananchi hao amesema kuwa wanaimani mradi huo wa maji utakuwa muaroabaini wa
tatizo la maji kwa manispaa ya Mpanda lakini kanuni na taratibu za kisheria
zifuatwe za kulipwa fidia wanannchi ambao maeneo yatapitiwa na mradi huo.
Kwa upande wake Penina Victor
ameeleza kuwa amekata tamaa kwakuwa tangu waanze kufatilia malipo hayo ya fidia
imekuwa muda mrefu sasa bila ya mafanikio yeyote.
Peter Matyampula mwenyekiti wa wahanga waliopisha ujenzi wa mradi wa Maji wa Miji 28 akizungumzia ucheleweshaji wa Malipo ya fidia kwenye Mradi huo. |
Mwajuma Ramadhani anaeleza kuwa
jambo hilo limekuwa kero kwao kwani kila siku wamekuwa wakilifatilia sula hilo
kwa muda mrefu sasahuku wakitumia gharama kubwa kwaajili ya kufatilia madai yao
ya fidia.
Anafafanua kuwa katika kufatilia
madai hayo wamekuwa wakipigwa dana dana na viongozi kwa kuwaahidi ahadi hewa
ambazo hazitekelezeki licha mthamini kuwaeleza kuwa baada ya uthamini fedha zao
zitalipwa baada ya miezi Sita kitu ambacho mpaka sasa hakuna kilichofanyika
zaidi ya kuendelea kusubiria.
Rafael changuvu amesema kuwa
hawako tayari kuona mradi huo ukiendelea bila ya kulipwa fidia zao kwa kuwa
imekuwa kero kwani wanananchi hao wanateseka na kuomba serikali kuwalipa fidia
kwa haraka.
Kufutia hali hiyo chombo hiki
kimemtafuta Rehema Nelsoni Kaimu
Mkurugenzi mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Manispaa ya Mpanda [MUWASA]
ameeleza kuwa uthamini kwaajili ya malipo ya wananchi hao umeshafanyika tangu
mwezi wa tano mwaka huu wa kuhakiki madai
yao.
Rehema amebainisha kuwa mchakato
wa malipo yao unaendelea chini ya Wizara ya fedha na wizara ya Maji na kuwaomba
wananchi hao kuendelea kuwa wavumulivu na hawezi kutoa majibu ya moja kwa moja
kuwa fedha hiyo italipwa lini.
Amewahakikishia wanananchi hao kuwa kila aliefanyiwa tathimini kwenye eneo lake atalipwa fedha yake na hakuna yeyote ambae hatolipwa fidia hiyo.