Na Paul Mathias-Katavi
Wafanyabiashara na wawekazaji katika mkoa wa Katavi wameombwa
kuchangamkia fursa za uwekezaji wa ndani kwa lengo la kuinua uchumi wa mkoa na
kuongeza kipato chao kupitia uwekezaji huo.
Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Albert Msovela akifungua semina ya Wawekezaji wafanyabiashara na wajasiliamali iliyoandaliwa na kituo cha uwekezaji Tanzania |
Wafanyabiashara na wawekazaji katika mkoa wa Katavi wameombwa kuchangamkia fursa za uwekezaji wa ndani kwa lengo la kuinua uchumi wa mkoa na kuongeza kipato chao kupitia uwekezaji huo.
Wito huo umetolewa na Felix Jonh Meneja uhamasishaji kutoka kituo
cha uwekezaji Tanzania [TIC]wakati akitoa semina kwa wafanyabiashara na wawekezaji
wa Mkoa wa Katavi.
Jonh ameeleza kuwa kituo hicho kipo katika kampeni ya kusimamia
kampeni ya uwekezaji wa ndani yenye lengo la kuhamasisha wafanyabiashara na
wadau wa sekta ya uwekezaji kujitokeza kufanya uwekezaji kwenye Nyanja
mbalimbali.
Amesema kuwa kituo cha uwekezaji Tanzania kimefika mkoa wa Katavi
kwa lengo la kukutana na wafanyabiashara wajasilaimali na Wawekezaji kwa lengo
la kutoa elimu na hamasa kwa kushirikiaana na wadau wa uwekezaji hususani
taasisi za kifedha.
‘’Tumeweza kuongea na wanakatavi naamini wametuelewa na wengi wapo
tayari kujitokeza kwaajili ya kusajili miradi yao ili waweze kunufaika na
vivutio vya kikodi’’-Felix Jonh
Amesema kuwa kwa kushirikiana na wadau wa uwekezaji kupitia kituo
cha uwekezaji Tanzania wawekezaji na wafanyabiashara kwa kuwapatia vivutio vya
kikodi na kuleta unafuu katika mitaji ya uwekezaji inayohitajika.
Amebainishakuwa wadau wa sekta ya uwekezaji ikiwemo taasisi za
kifedha zimekuwa msaada mkubwa katika uwekezaji kwa kuleta unafuu kwa
kuwawezesha watanzania kupata mitaji na
hatimae kufikia miradi ya ndoto zao.
Kwa upande wake Katibu tawala mkoa wa Katavi Albert Msovela
amesema serikali ya mkoa wa Katavi imekuwa ikiendelea kutengeneza mazingira
wezeshi kwa wawekezaji kwa lengo la kuvutia wawekezaji wengi zaidi kuja
kuwekeza Mkoa wa Katavi.
Msovela ameeleza kuwa maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali katika miundo mbinu mbalimbali ikiwemo Barabara,Maji na umeme imekuwa kivutio kikubwa cha wawekezaji kwa mkoa wa Katavi.
‘’Miundombinu ambayo inawezesha Viwanda viweze kuwepo kwa sababu
upatikanaji wa maji upo wa kutosha aridhi ipo ya kutosha na hivi sasa tunaenda
kuwa na umeme wa Grid ya Taifa kwahivyo tunawakaribisha wawekezaji
wote’’-Msovela
Amebainisha kuwa Mkoa wa Katavi unafursa mbalimbali za uwekezaji
ikiwemo Utalii, Mabonde mbalimbali ya Kilimo ambayo yanaweza kusaidia shughuli
za kilimo pamoja na aridhi yenye rutuba ambayo inakubalika kwa kilimo cha aina
yeyote.
Kuhusu fursa ya Masoko amesema mkoa wa Katavi nimiongoni mwa Mikoa
inayopakana na nchi za Congo,Burundi,Uganda na Rwanda hali hiyo hulahisisha
upatikanaji wa masoko wa bidhaa mbalimbali kwa wawekezaji wa Mkoa wa Katavi kwa
kufanya baishara na watu
Wenslauns Kamtoni mmoja ya wawekezaji waliodhuria semina hiyo amesema kuwa kupitia kituo cha uwekezaji Tanzania kimekuwa kiunganishi kwa wawekezaji kwa kuwasaidia wawekezaji kupata fursa za kuingia ubia wa uwekezaji na watu kutoka nje ya nchi.
Katika hatua nyiningine ameishukuru serikali kwa namna
inavyoendelea kuboresha miundombinu ya Barabara ili kurahisisha uchukuzi kwa
wawekezaji na wafanyabiashara kwa ujumla.
Sekta ya uwekezaji imekuwa ikitajwa kuwamoja ya sekta ambayo
imekuwa ikizalisha ajira nyingi kwa watanzania na kupunguza kwa kiasi flani
tatizo la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana