WATU WATANO WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO 18
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Watu sita wanashukiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa
Katavi kwa tuhuma za kukamatwa na
meno ya Tembo vipande 18 wakiwa wameyahifadhi ndani ya
nyumba katika maeneo ya Manispaa ya
Mpanda na Inyonga Wilayani
Mlele Mkoani Katavi na
bunduki mbili aina ya gobole pamoja na
nyama pori vipande 26.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Katavi David
Mutasya amewaambia Wandishi wa Habari kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa
kufatia msako mkali uliofanywa na jeshi
la Polisi Mkoa wa Katavi
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Devidi Mutasya akielezea kwa waandishi wa habari juu ya kamatwa kwa watuhumiwa watano wakiwa na meno ya Tembo vipande 18
Amesema watuhumiwa hao
watano walikamatwa na meno
ya tembo katika
maeneo mawili tofauti katika
eneo la Mtaa wa Ilembo Manispaa
ya Mpanda na
Inyonga Wilayani Mlele .
Mutasya ameeleza kuwa
kabla ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao jeshi la polisi lilikuwa limepata taarifa ya watuhumiwa hao kuwa wana jihusisha na maswala ya biashara haramu ya
meno ya tembo na ndipo baada ya kupata taarifa hizo jeshi la polisi lilianza
msako mkali wa kuwasaka na
waliweza kufanikiwa kuwakamata
watuhumiwa hao wakiwa na vipande 18 vya
meno ya tembo na bunduki
mbili na vipande 26 vya
nyama ori
Amebainisha kuwa
hadi sasa watuhumiwa hao bado wanaendelea kushikiliwa na jeshi la
Polisi Mkoa wa Katavi na
mara uchunguzi utakapokuwa umekamilika
watuhumiwa hao wanafikishwa Mahakamani ili wakajibu tuhuma ambazo
zinawakabili
Amesema katika kipindi
cha mwezi mmoja
wa Agosti Jeshi la Polisi limeweza kupata mafanikio mbalimbali kufatia doria ,misako na operesheni
walizofanya na kufanikiwa kukamatwa kwa watuhumiwa 97
wanaojihusisha na vitendo vya
uhalifu wakiwa na vielelezo mbalimbali
Amevitaja vielelezo
hivyo kuwa ni bangi kete 164, walizokamatwa nazo watuhumiwa 10, watuhumiwa 38 walikamatwa na pombe haranu gongo lita
281, watuhumiwa 17 walikamatwa kwa
kujeruhi watu na watuhumiwa 11
wamekamatwa katika matukio tofauti ya mauaji ,
Vilevile wameweza kuwakamata watuhumiwa 10 wakiwa na mali mbalimbali za wizi ambazo ni pikipiki mbili MC ,979 DJR na MC ,482 DVH na
mifuko 30 ya simenti yenye
thamani ya Tshs 1,800,000/
Kaimu Kamanda Mutasya
amewaonya wananchi wa Mkoa wa Katavi kutojihusisha na vitendo vyovyote vya uhalifu na ujangili
kwani watakao jaribu kufanya vitendo
hivyo watakamatwa mara moja na kuchukuliwa hatua sitahiki
MWISHO