KIMANTA ATANGAZA KUWA HANA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE

  

KIMANTA  ATANGAZA KUWA HANA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE 

Na Walter Mguluchuma
Katavi

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Idd Kimanta amekanusha uvumi ulio kuwa umeenea kuwa anampango wa kugombea nafasi ya ubunge katika uchaguzi 2025 katika Majimbo  mawili ya   Mpanda mjini na Mpanda vijijini yaliopo mkoa wa Katavi.

Kauli hiyo ya kutangaza kutogombea na fasi ya ubunge hapo mwakani ameitoa wakati alipo kuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.

 

Mwenyekiti CCM Mkoa wa Katavi akieleza mbele ya waandishi wa habari kuwa hana nia ya kugombea ubunge katika uchaguzi wa 2025

Amebainisha kuwa yeye ni mtu anae jitambua hivyo ataonekana ni mtu wa ajabu sanaa kwa nafasi alionayo ya unyekiti wa Mkoa halafu awe sehemu ya wagombea ni sawa na kuliacha goli la mpira wazi kwani moja ya majukumu alionayo ni kuwanadi wagombea watakao pitishwa na chama na kuhakikisha wagombea wote wa CCM wana shinda .

Kimanta amesisitiza na kuwataka wana CCM na wananchi wote wa Mkoa wa Katavi watambue kuwa yeye hana mpango wowote wa kugombea ubunge katika jimbo lolote la uchaguzi wala nafasi yeyote kwa sasa hivyo amewaomba wana CCM na wananchi kuwa watulivu kwani kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi watasikia mambo mengi ya upotoshwaji.




 Mwenyekiti CCM Mkoa wa Katavi Idd Kimanta akitoa ufafanuzi wa maswala mbalimbali mbele ya waandishi wa habari .
Amesema yeye na kamati zake za siasa za Mkoa na wilaya watahakikisha wana simamisha wagombea walio bora na wanao kubalika na wananchi na wata hakikisha wagombea hao wanashinda kutokana na kazi kubwa iliofanywa na serikali ya chama cha mapinduzi ikiongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

 

Kuhusu wagombea atakao wabeba ni wale tu watakao kuwa wameteuliwa na vikao halali vya chama cha mapinduzi Ccm yeye ndie atakae na sivinginevyo  na wala hana mgombea mwingine zaidi ya ambae atakuwa hajapitishwa na vikao halali vya chama.

Amesema hana mgombea yeyote anae muunga mkono kama ambavyo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakipotosha kwa hiyo mtu yeyote atakae pita mitaani akijitangaza kuwa yeye ni mgombea wa mwenyekiti wa Mkoa apuuzwe na wamfukuze.

 


Ametoa wito kwa wale viongozi waliopo madarakani waendelee kuchapa kazi kwani Chama na wananchi wana imani nao kutokana na    kazi nzuri walizo fanya na wanazo endelea kufanya .

MWISHO..

 

 

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages