Kiongozi wa mbio za mwenge Mwaka 2024 Godfrey Mzava akikagua daraja lililozinduliwa na MwengeNa Walter Mgulichuma-Mpanda
Mwenge wa Uhuru imezindua daraha la Kawaliyowa ambalo ambalolitakuwa ni mkombozi kwa Wanachi wa Manispaa ya Mpanda hususani wa Kata ya Ilembo na kuwaondolea wananchi adha waliyokuwa nayo hasa kipindi cha masika
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi akiishukuru serikali kwa kuleta fedha na kufanikisha daraja hilo
Mwenge wa uhuru unezindua Daraja la Kawaliyowa ambalolitakuwa ni mkombozi kwa wanananchi wa Manispaa ya Npanda hususani wa Kata ya Ilembo na kuwaondolea adha wananchi waliyokuwa wanaipata wakati wa Masika.
Uzinduzi huo umefanywa na kiongozi wa mbio za
Mwenge wa mwaka 2024 Godfrey
Mzava baada ya kuridhika na ujenzi wa
daraja hilo uliogharimu
kiasi cha shilingi
milioni 475,
Akitowa taarifa ya ujenzi wa daraja
hilo K aimu Meneja wa TARURA
wa Manispaa ya Mpanda
Mhandisi Pascal Sindani
amesema kuwa kukamilika kwa
daraja hilo muhimu kutakuwa na manufaa sana kwa wananchi wa Manispaa ya
Mpanda na ametaja baadhi ya
manufaa hayo kuwa ni
Kurahususha usafirishaji wa
nazao kutoka enei ka
Kawaliyowa kwenda katika
maeneo mengine ya Manispaa
ya Mpanda ambapo
hapo awali eneo
hilo lilikuwa halipitiki
wakati wa masika kiurahisi
na kuwafanya wananchi wapate adha
kubwa ,
Pia kutarahisisha
usafiri kwa wanafunzi wa shule za Msingi
na Sekobdari na wajawazito wanapokuwa wanakwenda kutafuta huduma
kwenye Zahanati na kwenye kituo
cha afya
kwani hapo awali walikuwa wanasubiri wakati wa nasika
maji yapungue ndipo wavuke m
Sindani
amesema uwepo wa daraja
hilo unatoa furusa
ya ajira kwa Vijana
kupitia shughuli za
Nodaboda awa biashara
hiyo ilikutana na
changamoto ya kutokuwepo kwa daraja kwenye
eneo hilo.
Kwa upande wake mbunge wa Jimbo
la Mpanda mjini Sebastiani Kapufi amemshukuru Rais Dk Samia suluhu Hassan kwa
kuwaletea fedha ambazo zimeweza kujenga daraja ambalo lilikuwa ni changamoto
wakati wa Masika kwa wananchi.
Amesema kuwa kukamilika kwa
daraja hilo itafungua fursa kwa wanananchi kufanya kazi zao za kiuchumi pasipo
na tatizo lolote na kuwaomba wananchi kuutunza mradi huo.
Kapufi amesema kuwa miradi ambayo
imekuwa ikiletwa na serikali imekuwa na tija kubwa kwa wananchi wa manispaa ya
Mpanda.
Kwa upande wake kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru Mwaka 2024 Godfrey Mzava amelidhishwa na mradi huo na kuwaomba wananachi kuutunza mradi.