WANANCHI KATAVI KUNUFAIKA NA MPANGO WA IMASA

Katibu wa Baraza la Taifa la uwezeshaji kiuchumi Beng'i Issa akielezea namna mradi wa IMASA utakavyo wanufaisha wananchi wa Mkoa wa Katavi kujiinua kiuchumi

 Na Paul Mathias-Katavi

Wananchi Mkoa wa Katavi wameobwa kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazotolewa na serikali kwa lengo la kuwawezesha kujiinua kiuchumi na kuwezesha kufikia malengo yao.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko[kushoto] akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph wakiifatilia kwa makini namna mradi wa IMASA utakuwa mkombozi kwa wananchi kujiinua kiuchumi

Wananchi Mkoa wa Katavi wameobwa kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazotolewa na serikali kwa lengo la kuwawezesha kujiinua kiuchumi na kuwezesha kufikia malengo yao.

Wito huo umetolewa na Katibu  wa baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi  Beng’i Issa wakati akizungumnza na wanananchi wa Mkoa wa Katavi wakati akielezea namna utekelezaji wa mradi huo utakavyo wanufaisha kujiinua kiuchumi.

‘’Leo tupo hapa Katavi kuutambulisha mradi wa kuimalisha uchumi na Mama Samia mradi huu ni nikwaajili ya kuwawezesha wanananchi kiuchumi ambayo inajielekeza kwa wanawake vijana na makundi maalumu wenye ulemavu pamoja na wazee’’ amesema Beng’i.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akiwa na Katibu wa Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Beng'i Issa wakiwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mpanda Social hall kwaajili ya kuzungumnza na wananchi kuhusu uwezeshaji kiuchumi
Ameeleza kuwa mradi huo utakelezwa katika mikoa yote Tanzania kulingana na uhitaji wa Mkoa husika kwa kazi zinazofanywa na wajasilimali na shuhguli husika za kiuchumi.

Ameeleza kuwa Mkoa wa Katavi nimiomgoni mwa mikoa inayofanya vizuri katika sekta ya kilimo pamoja na sekta nyingine ikiwemo uvuvi na Madini.

Amebainisha kuwa kulingana na kazi hizo  zinazofanyika katika mkoa wa Katavi wanatarajia mradi wa imarisha uchumi na Mama samia utakwenda kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwakuwa Mkoa wa Katavi unafursa nyingi za kiuchumi.

’Mradi huu wa IMASA tutakapo imaliza awamu hii tunakwenda kukaa na kuangalia vipaombele kulingana na wadau tuliokutana nao kwa kuzingatia mahitaji na kipaombele chao’’-Beng’i

amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ananianjema ya kuwasaidia wananchi waweze kupiga hatua kwenye maisha yao kunavitu ambayo tutataka mikoa ifanye na serikali kuu nayoitafanya ili wanananchi waweze kuinuka kiuchumi.

Amewaomba wanaanchi kuchangamkia fursa za uwezeshaji kiuchumi ambazo serikali imekuwa ikizitekeleza kwa lengo la kuwainua kiuchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akito hotuba yake kwenye utambulisho wa mradi huo ameziagiza Halmashauri zote za mkoa wa Katavi kuanzisha vituo vya uwezeshaji kiuchumi vitakavyo wasaidia wananchi kupata maelekezo ya fursa za kiuchumi zilizopo kwenye maeneo yao.

‘’Niwaagize Wakurugenzi na wakuu wa Wilaya tukitoka hapa pamoja na katibu tawala katika ngazi ya mkoa kwenda kuanzisha vituo vya uwezeshaji kwenye Halmashauri zote kwenda kuanzisha vituo vya uwezeshaji kiuchumi ili wananchi wetu wapate elimu na maelezo yanayohusu uwezeshaji kiuchumi’’-Mrindoko

Mrindoko ametoa rai kwa wananchi kuendelea kulitumia Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi kwenye shughuli zao za kiuchumi kwakuwa ndio kiunganishi kwa masuala ya uchumi na fursa kwenye maeneo yao.

Amewahakikishia wananachi wa Mkoa wa Katavi kuwa Mradi huo atahakikisha unafanikiwa kwa vitendo ili wanannchi wapate fursa ya  kutambua mahitaji ya shughuli za kiuchumi kwenye mkoa wa Katavi.

Fortunata Kabeja Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Katavi ameeleza kuwa mradi huo utakuwa mkombozi kwa wanananchi kiuchumi kwakuwa unaekwenda kutekelezwa katika ngazi ya chini ambapo wananchi watapata nafasi ya kubainisha shughuli za kiuchumi na kuwezeshwa na serikali kupitia mradi wa IMASA.

Amemshikuru Rais DK Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuwazesha wananchi kiuchumi hali itakayosaidia kuinua maisha yao ya kila siku kupitia shughuli wanazozifanya.

Mozes Mkubwa Mwenyekiti wa waendesha Bajaji Mkoa wa Katavi amesema fursa hiyo imekuja katika wakati muafaka kwakuwa vijana wengi wamejiari katika kazi hiyo huku wengi wao wakiwa hawamiliki bajaji zao.

Tutashukuru sana kama mradi huu wa IMASA utatugusa sisi Vijana tuliojiari katika sekta hii ya usafirishaji tuweze kupatiwa mikopo ya bajaji na tuendelee kufanya shughuli zetu vizuri.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages