MWENGE WA UHURU WAZINDUA SHAMBA LA MITI WILAYA YA TANGANYIKA

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Godfrey Mnzava akipanda Mti kwenye Shamba la Miti Kijiji cha Kagunga kama ishara ya kutunza Mazingira.

 Na Jackson Gerald-Katavi

Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2024 Godfrey Mnzava ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Kwa uhifadhi wa mazingira na kuwa kinara wa biashara ya hewa ukaa.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mnzava [kushoto]akizindua Shamba la Miti   Kjiji cha Kagunga Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi 

Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2024 Godfrey Mnzava ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Kwa uhifadhi wa mazingira na kuwa kinara wa biashara ya hewa ukaa.

Ameyasema hayo baada ya kuzindua shamba la miti  katika Zahanati ya Kijiji Cha Kagunga.

Mnzava amesema kuwa Wilaya ya Tanganyika imekuwa mfano kwa uhifadhi wa mazingira ndiyo maana imekuwa ya kuigwa kwenye biashara ya hewa ukaa.

"Huku hakuhitaji elimu kubwa sana ya utunzaji wa mazingira maana tayari mmekuwa vinara Kwa biashara ya Karboni nimeambiwa hapa zaidi ya Bilioni 14 mmepata fedha za hewa ukaa"Mnzava 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mnzava akihamasisha matumizi safi ya Nishati Mbadala kwa wananchi
Amewaomba wananchi kuendelea na utamaduni wa kutunza mazingira ili waweze kupata faida itokanayo na rasilimali misitu. 

Katika hatua nyingine Kiongozi huyo wa mbio za mawenge amegawa mitungi ya gesi 30 Kwa wananchi kama inshara ya kuunga mkono juhudi za serikali Katika matumuizi ya Nishati safi ya kupikia.

Amefafanua Kuwa wakati umefika Kwa wananchi kuanza kutumia Nishati mbadala ya kupikia ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

"Niwaombe sana ndungu zangu wananchi tuunge mkono juhudi za serikali Kwa kutumia Nishati mbadala ya kupikia mitungi hii iwe chachu Kwa kwenda kuwaelimisha wananchi wengine"Mzava.

Awali akitoa taarifa ya mradi wa Shamba la Miti Kijiji cha Kagunga Joseph Bisura ameeleza kuwa Shamba hilo linaukubwa wa Hekari moja ambapo jumla ya Miti 540 ya matunda, kivuli na Mbao imepadwa kwenye shamba hilo.

Amebainisha kuwa manufaa ya shamba hilo kwa wananchi wa Kijiji cha Kagunga kupata fursa ya elimu kuhusu uhifadhi ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi . 

Kuhusu juhudi za upandaji wamiti katika Halmashauri hiyo Bisura amesema kuwa kwa msimu wa 2023/2024 Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imefanikiwa kupanda miti 3,349,289 sawa na 223% yenye lengo la kufikia miti 2,846,895 sawa na 85 %.

Sulemani Moshi Kakoso Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini pamoja na Martha Mariki Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi kwa pamoja wamewaomba wananchi kuwa mfano bora kwa kuendelea kutunza mazingira kama sehemu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mradi wa Shamba la Miti Kijiji cha Kagunga ambao umetembelewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2024 .unagharimu kiasi cha Shilingi Laki Tisa [900,000]

Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa Mwaka 2024 unaenda sambamba na kaulimbiu isemayo Tunza Mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages