WAKULIMA KICHEKO WAITAJA NFRA MKOMBOZI KWA UNUNUZI WA MAZAO

Baadhi ya wakulima Mkoa wa Katavi wakiwa katika uuzaji wa zao la Mahindi katika Kituo cha ununuzi wa kituo cha mazao Mpanda chini ya usimamizi wa NFRA

Na Paul Mathias-Katavi

Wakulima katika Mkoa wa Katavi wameipongeza serikali kwa kuipa hadhi Wilaya ya Mpanda kuwa Kituo cha ununuzi wa Mazao mbalimbali kupitia Wakala wa hifadhi ya chakula hapa nchini [NFRA].

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumnza na wakulima kwenye kituo cha ununuzi wa Mazao Mpanda baada ya kutembelea kituoni hapo

Wakulima katika Mkoa wa Katavi wameipongeza serikali kwa kuipa hadhi Wilaya ya Mpanda kuwa Kituo cha ununuzi wa Mazao mbalimbali kupitia Wakala wa hifadhi ya chakula hapa nchini [NFRA].

Wakizungumza wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Katavi,  Mwanamvua Mrindoko alipoyetembelea maghala ya kuhifadhi Chakula ya NFRA kanda ya Mpanda wanananchi hao   wamesema bei ya Serikali inaridhisha tofauti na ile ya walanguzi.ambayo ilikuwa inawanyonya wakulima

 "Tunaishukuru Serikali kwa kuja na bei nzuri ya ununuzi wa mahindi ya Sh 700 kwa kilo moja  Sh 70,000 kwa gunia inasaidia kurejesha gharama tulizotumia katika uzalishaji na kukidhi  mahitaji ya maisha yake ya kila siku’’.-Joyce lufungule Mkulima

Samweli Mtambalike Afisa Mfawidhi wa NFRA Mpanda akitoa taarifa kwa mkuu wa Mkoa wa Katavi juu ya mwenendo wa ununuzi wa mazao kwenye kituo hicho

Ameeleza kuwa kupitia uwepo wa kituo hicha ununuzi wa Mazao wanawake pamoja na vijana wamepata fursa ya kufanyakazi ya kubeba mizigo huku akina mama wakipata fursa ya kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuchambua mahindi kwenye kituo hicho na kujipatia kipato

Mayunga Maganga,amesema kuwa hawakuwa na soko la uhakika la mahindi hali iliyofanya walanguzi kuwanunulia mazao ikiwemo Mahindi kwa kununua mahindi kwa Sh 47,000, kitu ambacho kiliathiri kipato chao.

‘’Kituo hiki ni mkombozi kwetu kwani kabla ya kituo hiki tulikuwa tunauza mahindi kwa walanguzi na kutu nunulia bei ya chini ila kwa sasa tunasema asante Rais Samia’’

 

Samweli Mtambalike Afisa Mfawidhi wa NFRA kanda ya Mpanda,  amesema wamepangiwa kununua tani 40,000 za Mahindi lakini tangu walivyoanza ununuzi zaidi ya Mwezi mmoja uliopita hadi sasa wamenunua tani 6,585.

Ameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kuweka kituo cha ununuzi wa zao la Mahindi na mazao mengine kwakuwa mkoa wa Katavi nimiongoni mwa mikoa inayozalisha kwa wingi

Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amewaomba wakulima kuongeza tija katika uzalishaji mazao ya nafaka ili waweze kupata ziada ambayo watawauzia NFRA ambalo ndilo soko la uhakika.

 

"Tuna wataalamu wa kilimo huu ndio wakati wenu wa kuwafikia wakulima vijijini na kuwa elimu ya kuzalisha kwa tija, sio kuongeza maeneo ya kilimo hapa nazungumzia eneo dogo ili uzalishaji mkubwa kwa maelekezo ya wataalamu"Mwanamvua Mrindoko.

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara ya kikazi Mkoa wa Katavi alikitanzanga kituo cha Mpanda kuwa kituo Rasmi cha ununuzi wa Mazao kwa Mkoa wa Katavi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages