Na Mwandishi wetu –Katavi.
Ufungaji
wa Mashine za kusaga unga na kukoboa mahindi katikati ya Makazi ya watu umeleta
changamoto nyingi,pamoja na kuwa mashine hizo zinatoa huduma muhimu kwa
jamii,uwepo wake unakuja na athari za kiafya na kiuchumi ambazo zinahitaji
umakini wa haraka kutoka mamlaka husika.
Kama inavyoonekana pichani ni moja ya
jengo ambalo mashine zimesimikwa karibu na makazi ya watu,Maendeleo ni muhimu
lakini tunapaswa pia kufikiria athari za mitetemo na vumbi vinavyotokana na
mashine hizi kwa jamii
Tukizungumzia
athari za kiafya, zinazotokana na mashine za kusaga unga, zinatoa vumbi linaloweza
kuathiri mfumo wa kupumua kwa watu wanaoishi karibu na Mashine hizo.Vumbi hilo
linaweza kusababisha magonjwa ya mapafu kama vile bronchitis na athari za muda
mrefu kama asthama.
Kuhusu
Mitetemo,Msingi wa Mashine hizo unazalisha mitetemo inayoweza kuathiri nyumba
zinazozunguuka ,mitetemo hii inaweza kuleta matatizo ya kiafaya kama maumivu ya
viungo na kuathiri ubora wa maisha kwa kuhamasisha wasiwasi na kutokuwa na
utulivu.
Kuhusu
Sauti kuu inayotokana na mashine hizi
inaweza kusababisha matatizo ya kusikia na kuongeza viwango vya wasiwasi kwa
wakazi wa eneo hilo.
Hiki ni
kinu cha moja ya Mashine za kusaga zinaleta mabadiliko,lakini pia changamoto za
mazingira kwa wakazi wa karibu ni wakati wa kutafakari suluhisho.
Hali hiyo
imewafanya wananchi wapaze sauti kwa Mamlaka
za kiutawala kulalamikia hali hii, ambapo
wanatarajia hatua kutoka kwa Mamlaka za
kiserikali kuanzia ngazi ya uongozi wa Serikali za Mitaa,Kata na Halmashauri
kuchukua hatua za makusudi kuepusha zahama hiyo.
Hata hivyo
Mamlaka husika zinaonekana kufumbia macho matatizo haya takribani ni miaka mine
sasa tangu kuwepo kwa mashine hizo hadi leo, hali ambayo inazidisha hasira kwa jamii.Mamlaka zinatakiwa kuchukua
hatua za haraka kuhakikisha mashine hizo zinahamishwa.
Tunaweza
kuendeleza uchumi lakini hatupaswi
kusahau kuhusu ustawi wa jamii,mitetemo na vumbi vinahitaji kushughulikiwa.
Kuhusu
ukaguzi wa Afya na usalama Mamlaka ya Afya
na OSHA yaani Occpational Safety and Health Administration zinapaswa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili
kuhakikisha mashine zinatumika kwa njia salama na kwamba wahusika wanasimamia
vigezo vya usalama wa Afya.
Kwa upande
wa Wataalam wa Mipango Miji,watu wa Ardhi wanapaswa kuzingatia mahali ambapo
mashine za aina hii zinaweza kuwekwa,ili kuzuia athari za namna hii.
Kuhusiana
na huduma za kijamii Mamlaka ya Kibiashara inapaswa kuhakikisha kwamba biashara
zote zinazotoa huduma zinazohusiana na mazingira, na afya ya umma kwa usahihi.
Moja wa
kijana anayeshughulika na mashine za kusaga zilizoko kwenye makazi ya wjamii,,jinsi
ya kupunguza athari za mashine hizi kwa wakazi tunahitaji majadiliano kuhusu
usalama na mazingira(.picha zote na maktaba)
Kwa
Mantiki hiyo basi uwepo wa mashine za kusaga unga na kukoboa mahindi katikati
ya makazi ya watu ni suala linalohitaji umakini wa haraka.
Athari za
kiafya,mitetemo na sauti kubwa vinawanyima wananchi haki yao ya kuishi katika
mazingira salama.
Hivyo basi
ni jukumu la Mamlaka husika kuchukua hatua za makusudi na za haraka ili kulinda
afya na ustawi wa jamii.
Wananchi
wanahitaji kuona hatua zikiwekwa ili
kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao ya kila siku kwenye makazi yao.