WANANCHI KUNUFAIKA NA UJENZI WA DARAJA LA MILIONI 500

 

Msitahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry[Mwenye shati la bluu] akiwa katika Daraja la Milala Shongo Kata ya Misunkumilo ambalo litaanza kujengwa hivi karibuni 
Na Paul Mathias-Mpanda

Msitahiki meya wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi Haidary Sumry ameipongeza serikali kupitia Wakala wa Barabara za Mnjini na Vijijini Tarura Wilaya ya Mpanda  kwa kuendelea kuboresha miundo mbinu ya barabara kwenye Manispaa ya Mpanda.

Msitahiki meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry akisiliza kwa umakini maelezo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni alipotembelea na kujionea ujenzi huo.

Msitahiki meya wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi Haidary Sumry ameipongeza serikali kupitia Wakala wa Barabara za Mnjini na Vijijini Tarura Wilaya ya Mpanda  kwa kuendelea kuboresha miundo mbinu ya barabara kwenye Manispaa ya Mpanda.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara ya kutembelea Miradi ya Daraja la Kingamboni Kata ya shanwe linalounganisha kata za Makanyagio na  Barabara ya Milala shongo Kata ya Misumkumilo.

Ameesema kuwa ujenzi wa Daraja hilo utaleta unafuu kwa shughuli za wananchi katika shughuli zao za kila siku kwakuwa wakati wa masika kumekuwa na changamoto kwa wananchi kutatiza shughuli zao.

Muonekano wa sasa wa Daraja la Milala shongo ambalo ujenzi wake utaanza hivi karibuni 
''Daraja hili likikamilika litakuwa mkombozi kwa wanannchi wetu na wanafunzi kuna wakati wanafunzi wetu walikuwa wanasobwa na maji lakini kwa hatua hii naimani kwa mwaka huu tataizo halitakuepo tena’’-Sumry

Ameishukuru serikali ya Rais Dk Samia Suluhu kwa kuona umuhimu wa kuleta kiasi cha shilingi Miloni 300  kwaajili ya ujenzi wa Daraja hilo.

Joseph Hoza Meneja wa Tarura Wilaya ya Mpanda amesema kuwa ujenzi huo wa Daraja hilo upo katika hatua ya kuridhisha na hadi kufikia Mwezi December Mwaka huu Daraja litakamilika.

Hoza amesema kukamilika kwa Daraja hilo litasidia wakazi wa Kata ya Makanyagio Shanwe na Misunkumilo katika shuguli zao za kila siku.

Mafundi ujenzi wakiendelea na ujenzi wa Daraja la Kigamboni Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi
Juma Ali Mkazi wa Kigamboni Kata ya Shanwe ameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga Daraja hilo huku akimuomba mkandarasi kukamilisha kwa haraka ujenzi huo kwakuwa kipindi cha masika kimekaribia.

‘’Masika hapa huwa ni bahari lakini serikali imetuona tunamshukuru Msitahiki meya kwa kututembelea na kujionea ujenzi huu kuna watoto wetu wakati wa masika walikuwa wananbebwa na maji hapa ila daraja hili likikamilika hapatakuwa na tatizo’’Ali

Katika ziara hiyo msitahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda ametembelea Barabara ya Misunkumilo hadi Milala shongo ambayo itaanza kujengwa hivi karibuni.

Msitahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda akiwa katika ukaguzi wa Daraja la kigamboni baada ya kutembelea kujionea mwenendo wa ujenzi wa mradi huo

Amebainisha kuwa katika vikao vya baraza la Madiwani kwa pamoja wamekubalina kuidhinisha kiasi cha Shilingi milioni 500 kupitia mfuko wa Jimbo kwaajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha changalawe pamoja na ujenzi wa daraja hilo.

‘’Kilio cha diwani wa Kata hii ya Misunkumilo kimekuwa cha muda mrefu amekuwa akipambana sana na sisi kwenye vikao vyetu tumekubaliana shilingi Milioni 500 za mfuko wa jimbo zijenge daraja hili ili wananchi wa Milala shongo wanufaike na serikali yao’’-Sumry.

Meneja wa Tarula Wilaya ya Mpanda Joseph hoza amesema kuwa ndani ya wiki moja mkandarasi atakuwa aeneo la ujenzi kwaajili ya kuanza ujenzi wa daraja hilo.

Anastazia Mashaka Mkazi wa Milala Shongo amesema ajisikia fahari kuwaona viongozi hao kwenye eneo hilo la daraja kwakuwa imekua kiuyao  ya muda mrefu daraja hilo kutengenezwa.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages