Kaim Mkuu wa Takukuru Stewart Kiondo akisoma ripoti ya robo ya kwanza ya julai hadi septemba 24 kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa katavi
KATAVI
Na Jackison Gerald
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) Mkoa wa
Katavi imefanikiwa kuzuia kiasi cha
shilling Milion kumi na nne, laki tano na arobain elfu (Sh. 14,540,000/=)
kutofanyiwa ubadhirifu na baadhi ya watumishi wasio waadilifu kutoka idara ya
fedha katika Halimashauri ya wilaya ya Tanganyika.
Akisoma ripoti ya utekelezaji wa majukumu katika robo ya
kwanza ya julai hadi septemba 24,Kaimu Mkuu wa Takukuru Stewart
Kiondo amesema fedha hizo zilitolewa na halimashauri hiyo katika akaunti ya
mapato kwa ajili ya kuwa kopesha wajumbe wa jumuia ya uhifadhi wa misitu ya
milima ya Ntakata(JUMININTA) iliopo katika halimashauri ya Wilaya ya
Tanganyika.
Amesema wajumbe hao walipatiwa fedha hizo kwa ajili ya kuwawezesha kuhudhuria maazimisho ya siku ya mazingira duniani mwaka 2024 ambayo kwa Tanzania yalifanyika Dodoma kuanzia tarehe 3/06/2024 hadi 6/07/2024.
Amebainisha kuwa ubadhirifu wa fedha hizo ulitakiwa
kufanyika kupitia akaunti ya mtu binafisi nasio katika akaunti ya halimashauri
ya wilaya hiyo.
Pia kiondo amesema katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Tanganyika Takukuru imefanikisha kurejesha mifuko 50 ya saruji yenye thamani ya shilingi Milion moja laki moja na ishirini na tano elfu(Sh.1,125,000/= ambayo iliazimwa na kiongozi wa Kata tangu mwaka 2023 na kugoma kuirejesha kulingana na makubaliano.
Sambamba na hayo amewaasa wazabuni wanao tumia mashine za(
EFD) ambazo hazijasajiliwa katika mfumo wa TRA na kuwasilisha bidhaa ambazo
Halimashauri zina lipa kwa kutoa risiti ambazo hazipo kwenye mfumo wa TRA kuwa
wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria.
Katika hatua nyingine Kiondo amebainisha kuwa Taasisi ya
kuzuia na Kupambana na rushwa (Takukuru )haito sita kuchukua hatua kali za
kisheria kwa watumishi wa serikali
wasiowaadilifu watakao shirikiana na wazabuni kuhujumu miradi ya maendeleo
inayo tekelezwa na serikali .
Kiondo ametoa rai kwa wananchi kuelekea uchaguzi wa serikali
za mitaa kutojihusisha na vitendo vya rushwa ambavyo wenda vikachangia kutopata
viongozi bora na wenye sifa kwaajili ya maendeleo ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Takukuru Mkoa wa Katavi imefuatilia miradi Thelathini na
Tatu (33) yenye thamani ya shilingi bilioni 46 katika sekta ya
elimu,Kilimo,Afya,uchumi ,Biashara na Miundombinu.
MWISHO