DC AONGOZA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WAPIGAKURA KWA VITENDO.

 

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph [kulia]akiandikishwa kwenye Daftari la Mkazi katika Mtaa wa Ikulu Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi 

Na Paul Mathias-Mpanda

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amewaomba wananchi wa Wilaya ya Mpanda kujitokeza Kwa wingi katika zoezi la unadikishaji wa Daftari la Mkazi Kwaajili ya kushiriki uchaguzi wa serikali za Mitaa.

Mkuu wa Wialya ya Mpanda Jamila Yusuph akitoa wito kwa wakazi wa Wilaya ya Mpanda kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kujiandikisha

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amewaomba wananchi wa Wilaya ya Mpanda kujitokeza Kwa wingi katika zoezi la unadikishaji wa Daftari la Mkazi Kwaajili ya kushiriki uchaguzi wa serikali za Mitaa.

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa wito huo baada ya kujiandikisha katika kituo Cha unadikishaji Cha mtaa wa Ikulu Kata ya Kawajense Manispaa ya Mpanda.

Jamila amesema kuwa Wilaya ya Mpanda imejipanga vyema katika zoezi Hilo la unadikishaji kwenye Maeneo yote ili wananchi wapate fursa ya kuwachagua viongozi wao wa mitaa na vijiji.

Amebainisha kuwa zoezi hilo limeanza Rasmi Tarehe 11/10/2024 na litakamilika 20/10/2024 Kwa Wananchi kujiandikisha kwenye vituo mbalimbali vya unadikishaji.

Ameeleza kuwa katika kipindi hicho cha siku kumi za unadikishaji wataendelea kutoa hamasa Kwa Wananchi ili wajitokeze Kwaajili ya kujiandikisha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli[kulia]akiwa katika kituo cha kujiandikisha mtaa wa Ikulu Kata ya Kawajense Manispaa ya Mpanda.
Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo wamesema wataenda kuwa mabalozi wazuri Kwa Wananchi ili kujitokeza Kwa wingi Kwaajili ya kujiandikisha.

Uchaguzi wa serikali za mitaa umepangwa kufanyika mnano 27/11/Mwaka huu ambapo wananchi watapata fursa ya kuwachagua viongozi wa mitaa,Vijiji,na vitongoji.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages