Na Paul Mathias-Mpanda
Mbunge
wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi amewaomba wananchi katika
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kujitokeza kwa wingi katika kuajimdikisha
katika Daftari la Mkazi ili wawaeze kushiriki katika uchaguzi wa serikali za
mitaa.
Mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini,Sebastiani Kapufi akiwa katika zoezi la kujiandikisha katika ofisi za mtaa wa Kichangani Kata ya Nsemlwa Mpanda Mjini
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi amewaomba wananchi katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kujitokeza kwa wingi katika kuajimdikisha katika Daftari la Mkazi ili wawaeze kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Wito
huo ameutoa baada ya kushiriki kujiandikisha katika ofisi za mtaa wa Kichangani
Kata ya Nsemlwa Manispaa ya Mpanda ambapo amesema nivyema wananchi kutumia
fursa ya kujiandikisha ili wawaeze kuwa sehemu ya kuwachagua viongozi kwenye
uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.
‘’Nitoe
wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kujiandikisha ili kupata tiketi ya
wao kutumia haki yao ya kikatiba ya kumchagua mwenyekiti wa mtaa,Mwenyekiti wa
Kijiji na Kitongoji na wajumbe wake bila kujiandikisha huwezi kuwa sehemu ya
kumchagua kiongozi wa serikali ya mtaa,,Kapufi
Ameeleza
kuwa fursa hiyo ya wananchi kujiandikisha katika daftari la mkazi kwaajili ya
uchaguzi wa serikali ni shemu ya namna ambayo serikali inaheshimu misingi ya
utawala bora kwa kuwahusisha wananchi moja kwa moja katika kuwachagua viongozi
wao kupitia sanduku la kura.
Amesema
kuwa zoezi hili ni tofauti na lililofanyika la urekebishaji wa kudumu la mpiga
kura kwakuwa lilikuwa linahusisha kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Rais Wabunge na
madiwani lakini zoezi hili linahusisha uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mwajuma
Haruna mkazi wa Mtaa wa Kichangani amesema kuwa ameshiriki kujiandikisha ili
aweze kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwaomba wananchi kujitokeza
kwa wimgi kwaajili ya kujiandikisha
‘’Nimefurahi
kujiaandikisha nina Imani nitashiriki katika uchaguzi wa kumchagua kiongozi
wangu wa mtaa bila tatizo lolote’’Mwajuma
Zoezi
la unadikishaji wa Daftari la Mkazi kwaajili ya kushiriki uchaguzi wa serikali
za mitaa limeanza rasmi leo 11/10/2024 na linatatalajia kukamilika 20/10/2024
huku uchaguzi wa serikali wa mitaa ukiwa umepagwa kufanyika 27/11/2024 hapa
mchini.