Na Paul Mathias-Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko
amezindua zoezi la uandikishaji la Daftari la wakazi Katika Mtaa wa Ilembo
Manispaa ya Mpanda kwaajili ya kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwamanvua Mrindoko[Mwenyekilemba cheusi] akiwa na wananchi wa Mtaa wa Ilembo katika foleni ya kuandikisha wananchi kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa. |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amezindua zoezi la uandikishaji la Daftari la wakazi Katika Mtaa wa Ilembo Manispaa ya Mpanda kwaajili ya kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa
Akizungumnza muda mchache baada ya kujiandikisha
kwenye mtaa huo mrindoko amesema zoezi
hilo limeanza leo 11/10/2024 na litakamilika mnamo 20/10/2024.
Ameeleza kuwa wahusika wataokaojiandikisha katika
Daftari la wakazi kwenye maeneo yao ni raia wa Tanzania wanaoishi katika
mitaa,Vitongoji,na Vijiji husika ili waweze kushiriki katika zoezi la uchaguzi
wa serikali za mitaa 27/11/2024.
![]() |
| Katibu Tawala Mkoa wa Katavi,Albert Msovela [kulia] akiandikishwa katika Daftari la Mkazi mtaa wa ilembo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi |
Mrindoko amewaomba wananchi katika maeneo
mbalimbali ya Mkoa wa Katavi kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili
waweze kutumia haki yao ya kikatiba kuwachangua viongozi wa mitaa na vijiji.
‘’Niwashukuru kwa wale wote ambao
wameshajiandikisha kwa takwimu tulizonazo hadi tunaondoka kwenye kituo hiki
tayari wananchi 55 wamejiandikisha huu ni mwanzo mzuri hii inaonyesha
nikwanamna gani wananchi wamehamasika ukiangalia muda wa saa moja tu watu hawa
tayari wamejitokeza’’ Mrindoko
Katika hatua hatunyingine amewaagiza wakuu wa
Wilaya kuongeza hamasa ya zoezi hilo kwa wananchi ili kuhakikisha wananchi wote
wanajiandikisha kwenye daftari la wakazi pasipo na changamoto yeyote.
![]() |
| Haule Jonh Mkazi wa Mtaa wa Ilembo Manispaa ya Mpanda akiandikishwa katika daftari la Mkazi ili aweze kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa. |
Kumbuli
ametoa rai kwa wanananchi kutumia siku hizo kumi kikamilifu kwa kujitokeza
kujiandikisha kwenye daftari hilo ili wapate fursa ya kushiriki uchaguzi wa
serikali za mitaa.
Ameeleza kuwa kunafaida ya kushiriki uchaguzi wa
serikali za mitaa kwakuwa kiongozi atakae mchagua atakuwa na uwezo wa kupanga
mipango ya maendeleo kuanzia ngazi ya mtaa na kijiji.
Uchaguzi wa serikali za mitaa umepagwa kufanyika 27,Novemba Mwaka huu nchinzima .




