Afisa uhusiano kwa wateja TANESCO Mkoa wa Katavi Proches Joseph akitoa elimu kuhusu matumizi mbalimbali ya umeme kwa wanafunzi wa Darasa la Tano Shule ya Msingi Mpanda |
Shirika la umeme Tanzania TANESCO
Mkoa wa Katavi katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja imezindua
maadhimisho hayo kwa kuanzisha klabu ya umeme Katika shule ya Msingi Mpanda
Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Katavi katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja imezindua maadhimisho hayo kwa kuanzisha klabu ya umeme Katika shule ya Msingi Mpanda Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Afisa uhusiano kwa Wateja TANESCO
Mkoa wa Katavi Proches Joseph amesema kuwa katika wiki ya Huduma kwa wateja
wameamua kuanzisha Klabu ya umeme shuleni hapo kwa wanafunzi wa Darasa la Tano
kwa lengo la kuhakikisha wanafunzi hao wanakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu
shirika la umeme na matumizi ya umeme kwa ujumla.
Amebainisha kuwa Elimu kuhusu
shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Katavi pamoja na huduma zinazotolewa
kwa wanananchi itakuwa sehemu ya Elimu itakayotolewa kwa wanafunzi hao ili wawe
mabalozi wazuri kuhusu huduma za umeme.
Ameeleza kuwa Klabu hiyo itakuwa ya kwanza kwa
Mkoa wa Katavi huku akibainisha kuwa mpango mkakati ni kuzifikia shule nyingi
zaidi kwa ajili ya kuwapatia elimu sahihi ya matumizi ya umeme wakiwa nyumbani
na maeneo mengine.
Afisa huyo amesema kuwa wamechagua kundi la wanafunzi wa
shule ya Msingi kwa kuwa wapo katika umri wa kujifunza mambo mbalilimbali hivyo
wakipatiwa Elimu hiyo watakwenda kuwa mabalozi wazuri wa kuisambaza elimu hiyo
kwa wengine na kuwasaidia zaidi katika umri wa utu uzima.Wanafunzi wa Darasa la Tano Shule ya Msingi Mpanda wakiwa katika Picha ya pamoja na maafisa wa TANESCO Mkoa wa Katavi baada ya kuanzisha Klabu ya umeme
“Tumechagua kundi hili la
wanafunzi hapa shule ya Msingi Mpanda kwa kuamini wanafunzi hawa wapo kwenye
umri sahihi wa kujifunza zaidi hivyo elimu hii kuhusu Tanesko itafika kwa
urahisi zaidi kupitia wanafunzi hawa”-Proches
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa
Shule ya Msingi Mpanda Michael Mwambojoke
amesema kuwa wamefurahishwa na ujio wa Taasisi ya TANESCO Mkoa wa Katavi
kwenye shule hiyo kwakuwa elimu hiyo itawasaidia wanafunzi watakao kuwa sehemu
ya Klabu ya umeme kufahamu zaidi kuhusu masuala ya umeme na nishati.
Mwambojoke ameziomba taasisi
zingine kuiga mfano wa TANESCO Mkoa wa Katavi kwa kuja na utaratibu wa
kuanzisha Klabu ya umeme yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi kuwa na uelwa
zaidi kuhusu umeme wakiwa Majumbani kwao.
‘’Tunawakaribisha sana TANESCO hapa
shuleni kwetu uanzishaji wa Klabu hii ya Umeme utasaidia kwa kuwa watoto hawa
watakuwa Mabalozi wazuri kuhusu TANESCO na watumiaji wazuri wa umeme wakiwa
nyumbani’’Mwambojoke
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa
Wateja huadhimishwa kila mwaka Mwezi Oktoba Dunia nzima kwa Mashirika ya Umma na Binafisi
kuelezea namna mashirika yanavyo hudumia wateja Maadhimisho hayo yanaenda
sambamba na kauli mbiu inayosema ‘’Ni zaidi ya matalajio’’.