Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko. |
Na Walter Mguluchuma, Katavi.
Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewaonya watu wote
wanao ishi katika Mkoa wa Katavi ambao sio
Raia wa Tanzania kutojihusisha katika kushiriki katika
uchaguzi wa Serikali za Mitaa .
Onyo
hilo amelitowa wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari
kuhusiana na maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika
Mkoa wa Katavi .
Amebainisha
kuwa Mkoa wa Katavi kutokana na asili ya Nchi yetu ya
kupokea wageni wa kutoka nchi jirani hali hiyo
imefanya Mkoa huu kuweza kupokea wageni wa kutoka
Mataifa mbalimbali wanao ishi kwenye Mkoa huu ambao sio Raia
wa Tanzania .
Kwa hali
hiyo anatowa onyo kwa watu ambao wanaoishi
kwenye Mkoa wa Katavi ambao sio Raia wa Tanzania
kutojihusisha kwenye uchaguzi huo kwa kuwa wao
hawana sifa ya kuhusika katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa
kupiga kura wala kugombea .
Mrindoko
amesema zoezi hili ilnawahusu Raia wa Tanzania tuu kwa
kuweza kujiandikisha na kupiga kura na kuchaguliwa ,
Amesisitiza kuwa
Serikali ya Mkoa wa Katavi itakuwa macho na kwa wale
watakao bainika kufanya udanganyifu wa aina
yoyote hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ,
Rc
Mrindoko amesema Mkoa wa Katavi utakuwa na vituo 835
katika ngazi za vitongoji ,Mitaa na Vijijivitakavyotumika
katika uandikishaji na upigaji wa kura katika uchaguzi wa Serikali za
Mitaa vilivyoko ,kwa Mkoa mzima .
Ametowa
wito kwa wananchi wote wa Mkoa huu kujitokeza kwa wingi
kuanzia tarehe 11 hadi tarehe 20
mwezi huu kujiandikisha kwa wingi kwa kuzingatia sifa za kuwa Raia wa
Tanzania kuwa mkazi wa eneo husika na kuwa na umri wa kuanzia
miaka 18 na kuendelea pia kuwa na akili timamu .
Amefafanua
kuwa zoezi ambalo lilifanyika mwezi julai mwaka huu la
maboresho la daftari la kudumu la maboresho ya tume
huru ya uchaguzi linahusika na uchaguzi mkuu
utakaofanyika mwaka 2025 kwa maana hiyo uchaguzi wa Serikali za
Mitaa wananchi wote wenye sifa ta kupiga kura watahitajika
kujiandikisha upya bila kujari kuwa wamehiandikisha kwenye daftari
la kudumu la mpiga kura .