![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko. |
Na Walter Mguluchuma, Katavi.
Wiki ya Mwanakatavi itafanyika Octoba 25, 2024 hadi Octoba 31,
2024 ambapo wananchi wa ndani nan je ya Mkoa wa Katavi watapata fursa kubwa ya
kujifunza na kuinua uchumi wao.
Mrindo amesema “Hii ni mara ya tatu tutaadhimisha wiki ya
Mwanakatavi ambayo lengo lake ni kumpatia mwananchi wa Mkoa wa Katavi fursa ya
kujifunza teknolojia mbalimbali zinazohusiana na sekta za kiuchumi, kijamii na
uzalishaji sambamba na kubadilisha uzoefu na mikoa na nchi mbalimbali kuhusiana
na fursa za kiuchumi, kijamii na uwekezaji”.
“Kuweza kuonesha bidhaa, maliasili na rasilimali tulizo nazo ndani
ya Mkoa wetu wa Katavi kwa wananchi wetu” Amesisitiza Mkuu wa Mkoa huo.
Ameweka wazi kuwa mwaka huu tukio hilo la mwanakatavi lina kauli
mbio “ Katavi Yetu Chagua Viongozi bora Imarisha
Uchumi kwa Maendeleo endelevu” ambapo ameeleza kuwa kauli mbiu hiyo inahamasisha
wananchi katika shughuli za uchumi na kuimarisha uchumi wao kwa kuongeza tija na
kuendelea kujivunza kutoka kwa watu wengine.
Ameongeza “Kwa kuwa ni mwaka mahususi kwa uchaguzi wa serikali
za mitaa pia kauli mbiu hii inasisitiza kuhimiza kila mwananchi kujitokeza na kushiriki
katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa maana hiyo nitumie nafasi hii kuwakaribisha
wananchi wa mkoa wa Katavi na nje kushiriki kwa pamoja”
Wiki ya mwanakatavi itakuwa na matukio mbalimbali kwa wiki
nzima ambapo kwa siku ya kwanza ya Oktoba 25, 2024 itakuwa ni siku ya ufunguzi na
yatakuwepo maonesho katika uwanja wa CCM Azimio Manispaa ya Mpanda Mkoani hapo.
Maonesho hayo yataanza asubuhi hadi saa moja jioni kila siku
kwa muda wa wiki moja na maonesho kwa maana ya kuonesha bidhaa, kujifunza
masuala ya fursa za uwekezaji, utalii, kilimo, mifungo, uvuvi, utamamduni wa
Katavi pamoja na upatikanaji wa fedha za kuichua uchumi.
Octoba 26, 2024 itakuwaa siku ya michezo na mazingira ambapo
kutakuwa na mbio zitakazo julikana kwa jina la Katavi Hip run zitakazo jumuisha
Km 5, Km 10 na Km 21 na kwenye mazingira kutakuwa na uhamasishaji wa utunzaji
wa mazingira na kuhamasisha masuala ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Octoba 27, 2024
itakuwa siku mifugo na uvuvi ambapo
washiriki watapata fursa ya kujifunza fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na
uvuvi.
Octoba 28, 2024 itakuwa ni siku ya uwekezaji na biashara ikihusisha
sekta za madini, viwanda, biashara za hotel na maduka na kutangaza sekta za
kifedha ambazo zinawawezesha wananchi katika shughuli za biashara na uwekezaji.
Octoba 29, 2024 itakuwa ni siku ya Utalii na Uhifadhi ambapo
kutakuwa na tukio maalumu la kuadhimisha miaka 50 ya Hifadhi ya Taifa Katavi na
kutembelea mbuga hiyo kama sehemu ya kufanya utalii.
Octoba 30, 2024 itakuwa ni siku ya Kilimo na Ushirika ambapo fursa
mbalimbali zitaonekana pamoja na kufanya tathimini ya mahala tulipo na waedapo
ili kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija.
Na Octobaa 31, 2024 itakuwa siku ya kilele ambapo mambo
yatakayo fanyika ni pamoja na kuzindua msimu wa akilimo wa mwaka 2024/25. Aidha
amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho hayo yenye fursa kubwa
kiuchumi.

