Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko (kushoto) akiwa na balozi wa Tanzania nchini Burudi Gelacius Byakanwa. |
Na Walter Mguluchuma, Katavi.
Balozi wa Tanzania Nchini Burundi Gelacius Byakanwa amewataka wa Tanzania na ukanda wa Afrika mashariki kutumia furusa za kitalii zilizopo katika Mkoa wa Katavi ambazo sehemu nyingine hazipatikani kabisa
Wito huo ameutoa wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa serikali wa Mkoa wa Katavi wakiongonzwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake Mkoani hapa.Balozi Byakanwa amesema kuwa fursa zilizopo katika Mkoa wa Katavi unaweza usikutane nazo kwingine tena hivyo unapofika katika Mkoa huo hakikisha unatumia fursa hizo za kipekee nahata kwa watumishi wanao fanya kazi za utumishi wasije wakamaliza utumishi wao bila kufanya kitu chochote.
Amefafanua kuwa katika ziara alioifanya ya kutembelea bandari ya Karema iliopo wilayani Tanganyika ameridhishwa sana na ujenzi wa bandari hiyo na anampongeza raisi Dr.Samia Suluhu Hassan kwakutoa fedha zaidi ya shilingi Bilion 47 zilizotumika kwaajili ya kujenga miundo mbinu ya bandari.
Bandari hiyo nisehemu nzuri sana kwaajili ya usafirishaji wa bidhaa zinazo safirishwa kwenda nje ya nchi na zinazo ingia nchini fursa alizo ziona ni ninyingi hivyo ameishauri mamlaka ya Mkoa wa Katavi waweze kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji badala ya mifugo ya ng’ombe na mbuzi kusafirishwa wakiwa wazima badala yake wajenge machinjio ya kisasa ili wawe wanauza kama nyama nakuongeza thamani kwa mfugaji.
Amefafanua kuwa hata kwenye uuzaji wa mchele nakopia wangeweza kuweka utaratibu wa kuwa na soko la kimataifa ambalo wakulima wetu watakuiwa wanauza kwa kuzingatia thamani ya soko la mteja anae peleka nje ya nchi na itapelekea kuongeza tija kwa wakulima .
Balozi Byakanwa amesema ziwa Tanganyika ni ziwa muhimu kwa nchi nne za DRC, Tanzania, Burundi na Zambia uwekezaji unaofanyika katika Ziwa Tanganyika unahitaji kuhusisha sekta zote zinazo husiana na uchumi wa bluu kama ambavyo ilivyo fanyika Tanzania Zanziba .
Amebainisha kuwa ziwa Tanganyika kuna fursa nyingi za kiutalii ambazo hazija fanyika hivyo kama Mkoa unapaswa kutengeneza mpango mkakati zaidi wa kuvutia wawekezaji na watalii kutoka nje ya mipaka ya nchi.
Amesema kunawatalii wengi sana wanao kuja kutembelea vivutio vilivyopo katika Mkoa wa Katavi na watalii wakizungu ambao amekuwa akikutana nao akiwa nchini Burundi wamekuwa wakiongelea vizuri sana Katavi kwani wanapokuwa wanaitaja Katavi wanaporudi makwao kila mtu huko anataka kujua Katavi kuna nini kwani ukiongelea Serengeti au Mlima Kilimanjaro hivyo tunalo jukumu la kuitangaza Katavi. Ili watu waweze kuijua zaidi.
Amesema kuwa Mkoa wa Katavi upo tayari kuhakikisha unakuza sekta za uchumi ,biashara na utalii kwa ajili ya kushirikiana nan chi ya Burundi katika suala zima la kukuza utalii na biashara na mawasiliano.
Amesema kuwa wanawakalibisha wawekezaji kutoka nchi ya Burundi kwakuwa tunaelewana nao zaidi lakini wanahitaji pia wawekezaji hata kama wanatoka china kwani wote ni wawekezaji wanawaribisha Katavi.
Muwekezaji kutoka nchini Burundi Fredi Nimubona amesema amegundua Katavi inavivutio vingi vya kitalii hivyo wawekezaji kutoka nje waweza kuona umuhimu wa kutumia fursa za kiuwekezaji kuwekeza Katavi.