UBORESHAJI MIUNDOMBINU SEKTA YA AFYA AHUENI KWA WANANCHI KATAVI

 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akiwahutubia wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri Mkoa wa Katavi 

Na Paul Mathias-Katavi

Mkoa wa katavi umepiga hatua katika ujenzi wa miundo ya afya kwa mwaka 2012  hadi 2024 kutoka vituo 79  Mwaka 2012 hadi kufikia vituo 149 ikiwa ni ongezeko la vituo 64 zikiwemo Hospitali za Wilaya vituovya afya na zahanati.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akifungua kikao cha 23  Kamati ya Ushauri Mkoa wa Katavi.

Mkoa wa katavi umepiga hatua katika ujenzi wa miundo ya afya kwa mwaka 2012  hadi 2024 kutoka vituo 79  Mwaka 2012 hadi kufikia vituo 149 ikiwa ni ongezeko la vituo 64 zikiwemo Hospitali za Wilaya vituovya afya na zahanati.

Akitoa taarifa ya Sekta ya afya katika kikao cha  23 kamati ya ushari wa  Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Katavi Katibu tawala Mkoa wa Katavi Albert Msovela amesema kumekuwa na ongezeko la miundombinu hiyo maradufu zaidi.

’Mkoa unahudumia jumla ya vituo 143 ambavyo vinatoa huduma ya afya katika mkoa wetu wa Katavi tunayo hospitali yetu ya Rufaa Mkoa wa Katavi lakini tunazo hospitali tano za Wilaya kwenye Halmashauri’’-Msovela

Katibu Tawala Mkoa wa Katavi,Albert Msovela akisoma taarifa ya miundombinu ya Afya ilivyoboreshwa na serikali Mkoa wa Katavi

Ameeleza kuwa vituo vya afya 28 kati ya hivyo 25 vinamilikiwa na serikali na 3 vinamilikiwa na watu binafsi pamoja na taasisi za dini huku akibainisha kuwa Mkoa wa Katavi unajumla ya zahanati 109 kati ya hivyo 91 zinamilikiwa na serikali na 18 zikiwa zinamilikiwa na taasisi za dini na watu binafsi.

Msovela amebainisha kuwa kumekuwa na ongezeko la vituo 64 ikilinganishwa na Mwaka 2015 ambapo mkoa wa Katavi ulikuwa na jumla ya vituo 79 vya kutolea huduma za afya.

Kuhusu hali ya watumishi katika sekta ya afya Msovela amebainisha kuwa hadi kufikia mwezi Oktoba ,2024 Mkoa unajumla ya watumishi 1492 kati ya Watumishi 4128 wanaohitajika katika mkoa mzima wa Katavi kwenye sekta ya afya.

Katika hatua nyingine ameishukuru serikali kwa kuwapatia watumishi 262 katika sekta hiyo ya afya wa kada mbambali  ambao wataenda kupunguza tatizo la watumishi kupitia vituo vyao vya kazi watakapo pangiwa.

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi akitoa mchango wake katika kikao cha Kamati ya ushauri Mkoa wa Katavi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua mrindoko ameishukuru serikali kwa kuendelea kuleta fedha kwenye miradi mbambali ya maendeleo ambapo kiasi cha Shilingi Trilioni 1.3 zimeletwa na serikali kwaajili kutekeleza miradi ya maendeleo

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages