Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrimdoko akifungua kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua
Mrindoko amewaomba Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa na Waziri wa Tamisemi Mohamed
Mchengerwa kuimalisha mtililiko wa fedha za ujenzi wa barabara katika Mkoa huo ili
kutowakwamisha wakandarasi katika
kutekeleza kazi zao .
Wenyeviti wa Halmashauri za Mkoa wa Katavi wakiwa katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewaomba Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa na Waziri wa Tamisemi Mohamed Mchengelewa kuimalisha mtililiko wa fedha za ujenzi wa barabara katika Mkoa huo ili kutowakwamisha wakandarasi katika kutekeleza kazi zao .
Mrindoko ametowa wito huo hapo jana wakati wa kikao cha 23 cha
bodi ya barabara ya Mkoa wa Katavi
wakati alipokuwa akisoma maazimio
yaliyopitishwa na kikao hicho
kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Katavi .
Akisoma maazimio ya
kikao hicho RC Mrindoko alisema anawaomba
mawaziri wawili wanaohusika na ujenzi wa Barabara Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Tamisemi mtililiko wa fedha uimalike zaidi ili fedha ziweze kufika
kwa ajiri ya miradi ili
kutowakwamisha wakandarasi kwenye
kutekeleza miradi yao .
Alisema kikao
cha bodi ya barabara
kinawaomba mawaziri hao wawili kufanya jitihada
zitakazo saidia ufikishaji wa
fedha katika Taasisi za TANROADS na
TARURA kwa ajiri ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara.
Aidha Mrindoko amewaagiza wakandarasi wote walioingia mikataba ya ujenzi wa barabara na madaraja kupitia Tanroads na Tarura na miundo mbinu mingine wahakikishe wanaanza kutekeleza miradi hiyo mara moja ili iweze kutekelezwa ndani ya muda wa mikataba yao inavyoelekeza ili iweze kukamilika na wananchi wa Mkoa wa Katavi waweze kunufaika .
Amebainisha kuwa bado
kwenye Mkoa huu imeonakana bado
kuna changamoto ya wizi wa vifaa vya
barabarani hivyo ametowa wito kwa wananchi
wahakikishe wanalinda na
kuhifadhi sana barabara hizo na madaraja na miundo mbinu mingine
inayohusiana na barabara kwani ni kwa manufaa ya wananchi wa Katavi na
Watanzania kwa ujumla .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mpimbwe Sailasi
Ilumba alisema kuwa hali ya barabara ya Kibaoni
Sitalike inayojengwa kwa kiwamgo cha lami ujenzi wake unasusua hivyo
anamashaka wakati wa kipindi hiki cha mvua hali ya barabara hiyo ikawa
mbata zaidi .
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Katavi Mwandisi Martin Mwakabende alieleza
kuwa kumekuwa na changamoto
kubwa ya wizi wa vifaa vya barabarani kama vile taa na uwekaji holela wa mageti ya kukusanyia ushuru .
Kuhusu barabara zenye changamoto
alieleza kuwa atawasiliana na wakandarasi ambao wapo
site ili wahakikishe maeneo yote ya barabara yanapitika kwa mwaka mzima pasipo kuwa na tatizo la kukwama .
Meneja wa Tarura wa Mkoa wa Katavi Mwandisi Innocemt Mlay wakandarasi wengi wanashindwa kumaliza kazi kwa wakati kutokana kutegemea kwaza malipo yao pindi wanapokuwa wamedai na wakisha lipwa ndio waendelee na kazi