WAFUGAJI WAPATIWA ELIMU KUTHIBITI WIZI WA MIFUGO

Mkuu wa Operesheni Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi na mrakibu mwandamizi wa Polisi [SSP]Juma Jumanne akitoa elimu ya ulinzi wa mifugo kwa wafugaji wa Wilaya ya Tanganyika

 Na Daniel Kimario -Katavi

Wananchi Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wametakiwa kujenga mazizi imara ya mifugo ili kuilinda mifugo yao na wahalifu ambao wamekuwa wakitumia udhahifu huo wa kufanya wizi wa mifugo.

Baadhi ya wafugaji Wilaya ya Tanganyika wakisikiliza elimu ya kukabiliana na tatizo la wizi wa mifugo kutoka kwa maafisa wa Polisi Mkoa wa Katavi.

Wananchi Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wametakiwa kujenga mazizi imara ya mifugo ili kuilinda mifugo yao na wahalifu ambao wamekuwa wakitumia udhahifu huo wa kufanya wizi wa mifugo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Katavi Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Juma Jumanne wakati akitoa elimu ya mazizi salama kwa jamii hiyo Katika Kijiji cha Majalila Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi.

Aidha, SSP Jumanne amewasihi wananchi hao kulisha mifugo yao katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya malisho na kuacha tabia ya kulisha katika mashamba ya wakulima ama kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi

Amekemea vikali kitendo cha wafugaji hao kuendelea kuwatumikisha watoto wadogo waliochini ya uangalizi kuchunga mifugo na badala yake wapelekwe shule.

Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Katavi Mrakibu wa Polisi John Mwaipungu ametumia fursa hiyo kuwasihi wafugaji hao kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika utoaji wa taarifa za wahalifu hasa matukio ya wizi wa mifugo kwa wakati ili kusaidia ufuatiliaji wa haraka na mifugo yao kuendelea kuwa salama.

Amesema suala ulinzi wa mifugo nilakila mmoja hivyo ni vyema kushirikiana kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kama kuna dalilia au viashiria vya wizi wa Mifugo.

Nao baadhi ya Wafugaji katika Wilaya hiyo wamelishukuru jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kuendelea kutoa elimu kwa wafugaji hao kuhusu umuhimu wa kujilinda na kutoa taarifa za wizi wa mifugo.

Wafugaji hao wamesema changamoto ya wizi wa mifugo wamekuwa wakikabilina nao huku wakiunda vikundi vya ulinzi shrikishi ikiwemo jeshi la Jadi Sungu sungu ili kutokomeza uhalifu huo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages