Washiriki wa Mafunzo yaliyoandaliwa na TAMCODE walipotembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti na Karanga Don King kilichopo Kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda. |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Mafunzo yaliondaliwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya jamii Tanzania (Tamcode) kwa kipitia mfuko wa UNESCO Alwaleed Philanthropies yaliofanyika Mkoani Katavi yameanza kuzaa matunda kwa mfanya biashara wa kiwanda cha kukamua mafuta ya Alizeti,Pamba na Karanga kuwa na mpango wa kunua Mashine ya kukamulia mafuta ya Karanga.
Washiriki wa Mafunzo hayo wakisalimiana na Mwekezaji wa kiwanda hicho Daniel Tarimo walipofika kwenye kiwanda chake.
Mafunzo hayo ya siku mbili yalitofanyika hivi karibuni katika
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi
yaliwashirikisha Waandishi wa
Habari,Wasanii wa kutoka chuo Kikuu cha Dodoma
na wadau wa utamaduni wa Mkoa wa
Katavi yenye lengo
la kuibua Urith wa Utamaduni usio shikika ili kuvutia wawekezaji
na kukuza fursa za kiuchumi.
Mwekezaji wa kiwanda cha
kukamua mafuta ya Alizeti ,Karanga
na Pamba Daniel Tarimo(Don King) kilichopo manispaa ya Mpanda
Mkoa wa Katavi amesema kuwa kutokana na ziara iliyofanywa na washiriki wa
mafunzo yaliyoandaliwa TAMCODE walipofika kiwandani hapo yamempa hamasa ya
kuona umuhimu wa kununua Mashine inayochakata mafuta ya karanga.
Amesema awali kabla ya
kutembelewa na washiriki hao alikuwa anatumia Mashine ambayo ni maaalumu
kwaajili ya kukamua mafuta ya Alizeti kwaajili ya kukamulia mafuta ya Karanga
jambo ambalo ameliona siyo sahihi.
Tarimo amebainisha kuwa kwa sasa hali ya mahitaji ya mafuta ya Karanga imekuwa kubwa ndani ya Mkoa na nje ya nchi kwa ujumla hivyo kutokana na ongezeko la mahitaji na hamasa aliyoipata imemlazimu kufanya utaratibu wa kuagiza mashine nje ya nchi kwaajili ya kukamulia mafuta hayo peke yake ikiwa sehemu ya kukuza uchumi.
Amefafanua kuwa uhitaji huo
unachangiwa pakubwa na serikali kutengeneza mazingira wezeshi kwa wawekezaji
kupata fursa ya kuongeza wigo wa kutoa huduma hizo kwa wanannchi kutokana na
uwekezaji husika hususani wananchi wengi walikuwa wameshasahau utumiaji wa
mafuta ya karanga ambayo ni salama zaidi kwa watumiaji.
Awali wakati wa funzo hayo Dk Deograsian ngulu Mhadhili wa chuokikiuu cha Dodoma ameishukuru TAMCODE kwa kuwakutanisha na wanahabri ili kufanya kazi kwa pamoja kupitia mafunzo ambayo yatakuwa na manufaa kuhusu urithi wa utamaduni usioshikika.