BHSF SONGAMBELE FOUNDATION
Na Walter Mguluchuma
Katavi .
Taasisi ya BHSF (SONGAMBELE FOUNDATION) imewasihi wazazi na watu wote kwenye Jamii ambao wanawatoto wenye mahitaji maalumu wasiwachukulie watoto hao kuwa ni shida na laana kwenye jamii na wasitumie mila potofu kama mtaji wa kuwaharibu zaidi kwani baadhi ya wazazi wana Imani potofu kuwa watoto hao ni sehemu ya kujipatia kipato .
Wito huu umetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya BHSF (SONGAMBELE FOUNDATION ) Thomas Songambele) inayojishughulisha na kuwaunganisha watoto wenye mahitaji maalumu ya kiafya kwa ajiri ya kupatiwa matibabu wakati wa hafla ya mwaka ya kuishukuru Taasisi hiyo na wadau mbalimbali kwa kazi kubwa wanayo fanya .
Mkurugenzi wa Songambele Foundation Thomas Songambele akielezea Taasisi hiyo inavyo wa unganisha watuwemye mahitaji maalumu jinsi inavyo shirikiana na wadau katika kuwasaidia kupata huduma ya matibabu.
Songambele ametaja baadhi ya shughuli wanazo fanya kwa kushirikiana na wadau ni kama vile kuwapeleka kwenye matibabu watoto wanao zaliwa na vichwa vikubwa , mdomo sungura , matege ya nje na ndani mgongo wazi na wale wanaopata tatizo wakati wa kuzaliwa mtoto asiye kaa, shingo kukaza wasio omega hao wote wanawahudumia.
Amebainisha kuwa hayo ndio wamekuwa wakiyafanya na kwa mwaka huu wameisha wapeleka hadi sasa watoto 20 kwa ajiri ya matibabu katika hospitali za Rufaa zinazotowa huduma ya matibabu hayo ikiwepo hospitali ya Rufaa ya KSMC ya Mkoani Kirimamjaro .
Kuhusu taasisi hiyo na mwelekeo wao kama ilivyoanza ni kwa ajiri ya watoto wasio jiweza cha kwanza awe asemi , awe atembei awe hana utambuzi kama watoto wengine ambao tunapaswa kumwona nao kama walivyo watoto wengine .
Wazazi wakiwa na watoto wao wenye mahitaji maalumu wakati wa hafla ya kuishukuru taasisi ya Songambele Foundation na wadau mbalimbali walio wezesha kufanikisha matibabu ya watoto ambapo kwa mwaka huu jumla ya watoto 20 wamepatiwa matibabu kwenye Hospitali za Rufaa KSMC na CCBRT.
Amewasisitiza wazazi na watu wote kwenye jamii ambao wana watoto wenye mahitaji maalumu watambue kuwa watoto hao sio laana na wasiwachukulie kuwa ni shida kwenye familia na pia mila potofu zisichukuliwe kuwa ni mtaji kwani baadhi ya watu wanaimani potofu za kuwa ukimuua mtoto mwenye ulamavu utapata fedha na mali hiyo ni hapana.
Amesisitiza wazazi na walezi wenye watoto wa namna hiyo wawapeleke kwenye shirika hilo wao watawasaidia na sehemu yoyote ambayo watamwona mtoto mwenye matatizo hayo wawaomyeshe kwenye shirika hilo ili waweze kuondolewa changamoto zao kwa kupelekwa kwenye matibabu Hospitalini .
Amefafanua kuwa watoto wenye mahitaji maalumu na watoto kwa jumla malezi yamepungua sana na baadhi ya wazazi wamebaki kusema jeshi la polisi likazuie ukatili jambo ambalo sio sahihi kwani jukumu la kuwalea watoto lipo kwenye jamii hivyo wao ndio wenye wajibu wa kwanza wa kuwalea watoto wao na wawe mabalozi wa kuwalea watoto hao .
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu wa Mkoa wa Katavi Anna Shumbi ofisi yake inafahamu kazi kubwa inayofanywa na taasisi hiyo na hivyo watu wanapaswa kuiona kazi hiyo sio ya Songambele Foundation peke yake bali ni kazi ya kila mtu anapaswa kuifanya kwa nafasi yake hivyo tunapaswa kuitambua kazi wanazo fanya na tuwaige .
Afisa Mkuu wa maendeleo ya jamii Anna Shumbi akiwahutubia wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalumu katika hafla iliofanyika katika kituo cha songambele foundation.Amesema watoto wenye mahitaji maalumu wanayo haki sawa kama ilivyo kwa watoto wengine ya kupata malezi mazuri na pia kulindwa na vitendo vya ukatili na wanayohaki ya kujifunza na kupata elimu kwa hivyo sio sawa kiwaficha nyumbani watoto wenye mahitaji maalumu n ahata kutotaka watu wasijuwe kama una mtoto mwenye mahitaji maalumu hiyo haikubaliki katika ulimwengu wa sasa.
Shumbi amesema Serikali ipo kuanzia kwenye ngazi za chini kwa hari hiyo ni jukumu la kila mtu kuwaibua watu wenye mahitaji kwenye maeneo yao na kujua mahitaji yao na kuwafikisha kwa Songambele Foundation ambao wapo kwa ajiri hiyo .
Nae Geturda Mlokozi ambae ni mama wa watoto wawili mapacha amesema watoto wake walizaliwa wote wawili wakiwa na matege na walikuwa wakitembea kwa shida baada ya muda wakawa wameshindwa kabisa kitembea na vifua vyao vilikua vikubwa .
Ameeleza kuwa kufatia changamoto hiyo alilazimika kwenda kuwasiliana na Taasisi hlyo ambayo ilimsaudia kumuunganisha na wadau wake na kuweza kupatiwa matubabu watoto wake wote wawili ya upasuaji na sasa hivi wote wawili wanatembea kama kawaida