Msitahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry akiongoza kikao cha baraza la Madiwani |
Na Paul Mathias-Mpanda
Baraza la Madiwani
katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda limewaomba wakuu wa idara wa
halmashauri hiyo kufanyia kazi changamoto ambazo zimekuwa zikiibuliwa na
madiwani kwenye vikao vyao ili kuwasaidia wananchi kutatua kero zao.
Baadhi ya Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wakiwa katika Kikao hicho. |
Hayo yamejili
katika kikao cha kwanza cha Robo ya kwanza ya Mwaka ya baraza la Madiwani
2024/2025 ambapo madiwani hao wamesema kuwa kumekuwa na maagizo mbalimbali
ambayo yamekuwa yanatekelezwa kwa kusuasua.
Akitoa
taarifa ya Kata ya Magamba Diwani wa Kata hiyo Fortunatus Chiwanga amesema
tatizo la kujengwa kihohela kwa vituo vya kuchenjua madini kwenye kata yake
imekuwa tatizo la muda mrefu licha ya kutoa taarifa hiyo katika vikao
vilivyopita.
‘’Mimi
niombe watalamu wachukue ushauri wa baraza kwa hili msitahiki meya nitakuwa
siwalishi taarifa kila kikao nawasilisha hoja hii ila majibu ya watalamu ni
mepesi sana’’-Chiwanga
Chiwanga ameiomba halmashauri kupitia watalamu wake kufika kwenye kata yake hususani maeneo ya uchimbaji ambayo yamekuwa yaki lalamikiwa na wananchi kwa raia wa Kigeni kujiingiza katika shughuli za uchimbaji bila utaratibu.
‘’Ukifatilia
watu wa Madini watakwambia watu wa mazingira tumeshamalizana nao ukija kwa
wananachi malalamiko sasa watalamu wanatuchanganya’’-Chiwanga
Kwa upande
wake Diwani wa Kata Shanwe Hafidhi Masumbuko akichangia taarifa ya Kata ya
Mpanda Hotel ameutupia lawama uongozi wa Halmashauri kwa kushidwa kuboresha
mazingira ya Machinjio ikiwemo kujenga choo na huduma ya maji ya uhakika.
‘’Hii
changamoto ya ukosefu choo eneo la machinjio tunaizungumnzia kila siku katika
eneo linalohitajika usafi ni eneo la machinjio kata kila siku wanawasilisha
hoja hii lakini utekelezaji hakuna’’-Hafidhi.
Deodatus Kangu Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda akijibu hoja mbalimbali za madiwani kwenye kikao hicho |
‘’Juzi tumeshidwa kuchinja hapa kwaajili ya ukosefu wa maji na huu ni mradi wetu Halmashauri sijui tunashidwa wapi’’-Hafidhi
Mstahiki meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry amewaonya wakuu wa idara wazembe kuwajibika kwa kutatua changamoto hizo kwakuwa maeneo yenye changamoto hizo zinafahamika.
‘’Itakuwa ni
jambo la ajabu sana afisa mifugo upo pale machinjioni unaona changamoto hiyo
ila hutoi taarifa sahihi ila anasubiria diwani aje kujenga hoja kwenya baraza
hili’’-Sumry.
Amewaomba wakuu wa idara kuwajibika ipasavyo kwenye nafasi zao ili kumsaidia mkurugenzi na wananchi wa manispaa ya Mpanda kwa ujumla.
‘’Wakuu wa
iadara baraza hili linamamlaka nao siku nikichachamaa hapa tuseme idara fulani
inashida patakuwa hapa toshi hapa kwahiyo tukawasaidie wananchi’’
Deodatus
Kangu Kaimu Mkrugenzi wa Manispaa ya Mpanda amesema watayafanyia kazi
changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza kwenye vikao mbalimbali vya baraza
hilo.