Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Stewart Kiondo akifungua kikao kazi cha kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya siasa vya Mkoa wa Katavi ili kuwa na uelewa wa kupinga rushwa katika kuelekea uchaguzi wa 2024/2025
Na Walter Mguluchuma
Katavi.
Taasisi ya
Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imewapatia mafunzo viongozi wa vyama vyote
vya siasa vilvyopo katika Mkoa wa Katavi juu ya utaratibu bora
wa kuelimisha wananchi pamoja na
wanachama wao madhara ya rushwa ikiwa nikatika kuelekea uchaguzi wa 2024
na 2025 na hatimae wananchi waunge
mkono mapambano dhidi ya Rushwa ya
kisiasa wakati wa uchaguzi .
Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuhudhuriwa na viongozi wa vyama vya siasa wa ngazi ya Mkoa na Wilaya .
Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Stewart Kiondo amewaambia washiriki wa mafunzo hayo ya siku moja kuwa lengo la kuwapatia mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo juu ya utaratibu bora
wa kuwaelimisha wananchi na
wanachama wao ili wajuwe madhara ya Rushwa wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi .
Viongozi wa vyama vya siasa wakiwa kwenye kikao cha kuwajengea uwezo namna ya kupinga rushwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi wa Raisi wabunge na madiwani 2025.
Amesema Takukuru Mkoa
wa Katavi wanaendelea kuweka
mikakati ya pamoja pamoja na vyama vya siasa na wadau
mbalimbali ili kuwa na mkakati wa pamoja
ili waweze kusaidiana kuzuia
Rushwa za siasa na Rushwa
nyingine .
Kiondo ameeleza
kuwa mafunzo hayo
yatasaidia pia kupata uzoefu
wa mchango wa vyama
vya siasa katika kuzuia
na kupambana na Rushwa pamoja na kuweka mikakati ya
pamoja katika kuelekea uchaguzi wa
Serikali za Mitaa 2024 pamoja na uchaguzi wa Rais Wabunge na madiwani 2025 hicho ndicho kikubwa wanachokitegemea kupata ushirikiano
na kuweza kutatua matatizo
hayo ya Rushwa .
Hivyo
wanapoelekea kwenye chaguzi hizo wanapaswa kubadilika kutoka
kuiona Rushwa kama
jambo la kawaida na waanze kuiona Rushwa
kama janga lililovamia nchi na lipo
katika jamii yetu likiwa
na madhara ya kuleta umasikini
katika nchi yetu .
Mchunguzu Mwandamizi wa
Takukuru Mkoa wa Katavi Leonard
Minja amesema Takukuru wataendela
kutowa elimu kwa wananchi kuhusu Rushwa
na madhara yake kwa
kuwa Tanzania inahitaji
kuwa na wananchi wazalendo wasio
jihusisha na Rushwa .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Mwanamvua Mrindoko amevishukuru vyama vya siasa kwa kuweza
kujitokeza kushirika kwenye
uchaguzi huu wa serikali za Mitaa
kwa wagombea wao kuchukua fomu na kuweza kuzirejesha .
Katibu wa siasa
na uenezi wa
Ccm Mkoa wa Katavi Teonas
Kinyonto ameviomba vyombo ambavyo vinasimamia ulinzi na
usalama katika Mkoa wa Katavi vihakikishe vinasimamia usalama ili ichaguzi uwe wa amani
.
Na Erasto Wegolo katibu wa chadema Mkoa wa Katavi ameitaka Takukuru wakati wa kipindi hiki cha uchaguzi
wanapokuwa wamepokea malalamiko ya
tuhuma za Rushwa wahakikishe wanazitatua kwa wakati .
MWISHO