Na Walter Mguluchuma
Katavi .
Ofisi ya Utamaduni Mkoa wa Katavi wameomba wananchi wa mkoa wa Katavi na Watanzania kwa ujumla
kumuunga mkono msaninii chipuzi
Francis Kinyonto maarufu (CHETTA-FLAYEE )aliyechaguliwa
kushiriki Tuzo ya Wasanii chipuzi wa
kizazi kipya wa Afrika
Mashariki itakayo fanyika Nchini Kenya.
Akizungumza na
Wandishi wa Habari kwa niaba ya Afisa
utamaduni wa Mkoa wa Katavi Afisa utamaduni wa Manispaa ya Mpanda Bakari Hamza
amesema kama Serikali wamefurahi na kumuona msanii CHETTA- FLAYEE kuweza kuchaguliwa kuwa
mshiriki wa Tuzo ya wasanii chipukizi
wa Arika Mashariki .
Afisa utmaduni Manispaa ya Mpanda Bakari Hamza akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msanii Chetta-flayee kushiriki tuzo za made in East music and media awards .
Amebainisha kuwa lengo la Serikali ya Mkoa wa Katavi ni
kuwainua wasanii vijana wa Mkoa wa Katavi
ili kazi zao wanazofanya ziweze
kuonekana ndani ya nchi na nje ya nchi kama
alivyofanya CHETTA – FLAYEE.
Hamza amesema Serikali ya Mkoa wa Katavi wamefurahi sana na
watakuwa bega kwa bega na msanii huyo
katika ushiriki wake wa tuzo hiyo ya
Afrika Mashariki ili aweze
kufanikisha kwenye ushiriki wa
mashindano hayo na pia amewaomba Watanzania wote na
wasio Watanzania kumpigia kura
ili aweze kuwa mshindi wa mashindano hayo.
Kwaupande wake Francis Kinyonto (CHETTA-FLAYEE) amesema kushiriki
tuzo hizo ni sifa
na nafasi ya kipekee inaonyesha jinsi ambavyo kazi zake zinavyowafikia watu zinavyothaminiwa .
Amewaomba wananchi wa Mkoa wa Katavi na Watanzania kwa ujumla
kuweza kumuunga mkono ili aweze
kupeperusha vema bendera ya nchi na kuweza
kuwa mshindi wa tuzo hizo ambazo
mwisho wake wa kupiga kura ni Desemba 5
MWISHO