Na Daniel Kimario, Afisa Habari Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi.
Katika kuelekea kilele cha siku 16 za kupinga ukatili Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na Dawati la jinsia na watoto wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi.
Akikabidhi msaada huo Desemba 8, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani amebainisha kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limeona ni vyema kufanya matendo ya huruma kwa wagonjwa hao ili wasijione wapweke, ambapo ameendekea kueleza kuwa Jeshi hilo linaendelea kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.Msaada uliotolewa kwa wagonjwa hao ni pamoja na taulo za kina
mama, pempasi, sabuni, sukari, unga, mafuta ya kupaka, miswaki na dawa za meno.