Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwenye Halmahauri kuu ya CCM Mkoa wa Katavi. |
Na WalterMguluchuma-Katavi
Ujenzi wa Barabara wa kiwango cha lami
ulianza kujengwa kutoka Mpanda kuelekea katika Bandari ya
Karema unatarajia kuwezesha Bandari ya Karema kuweza kufanya kazi
kwa ufanisi zaidi kuliko ilivyo sasa hivi kwani itasaidia
kusafirisha mizigo katika kipindi chote cha mwaka mzima kuliko ilivyo
sasa .
Ujenzi wa Barabara wa kiwango cha lami ulianza kujengwa kutoka Mpanda kuelekea katika Bandari ya Karema unatarajia kuwezesha Bandari ya Karema kuweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko ilivyo sasa hivi kwani itasaidia kusafirisha mizigo katika kipindi chote cha mwaka mzima kuliko ilivyo sasa .
Kauli hiyo ya Serikali ya Mkoa wa Katavi imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Mendeleo ya Ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Katavi kilichofanyika katika ikumbi wa Manispaa ya Mpanda .
Rc Mrindoko amesema Serikali imeweza kuweza katika Bandari ya Karema ambayo imekamilika kwa gharama ya zaidi ya Bilioni 48 wanaendelea kuisadia mpaka hapo itakapoweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi mara baada ya kukamilika kwa miundo mbinu ya Barabara.
Amebainisha kuwa watu wote wanafahamu kuna tatizo la Babara
lakini Serikali imeisha weka wakandarasi wawili katika vipande
viwili na tayari wakandarasi wapo kazini kwa ujenzi wa barabara
hiyo kwa kiwango lami na ujenzi huo umeisha anza .
ujenzi wa barabara hiyo kwenda Bandari ya Karema
utawezesha bandari yetu kuweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi
kuliko ilivyo sasa hivi kwa sababu
itatuhakikishia uwezo wa kusafirisha mizigo ya kwenda
Bandarini na kutoka kwenda kwenye Babdari ya Karema kwa ajiri ya usafirishaji
wa mizigo kwenda Nchi ya DRC
Ambapo kwa upande wa kilimo kwa mwaka 2023/2024 Mkoa wa Katavi umeweza kupata mafanikio makuwakwa kuvuna jumla ya Tani milioni 1,43 za mazao ya kilimo ya chakula na biashara kwa mwaka huu wa 2024/2025huu wa kilimo Mkoa unamalengo ya kuvuna zaidi yani Milioni 1,4 ya mazao ya chakula ma biashara
Mrindoko amesema upande wa utalii Mkoa uweza
kufanikiwa kwa kupata mafanikio makubwa kwa kuweza kuitangaza Hifadhi ya
Katavi na vivutio mbali mbali vilivopo katika Mkoa huu na waweza kuwa na
maonyesho ya Mwana Katavi ambayo ndani yake yanamaonyesho ya utalii
wanyama na ngoma za asili na wanatowa elimu mbalimbali kihusu utunzahi wa
misti vyanzo vya maji na maeneo yaliyohifadhiwa kwa mujibu wa
sheria .
Kwa upande wa sekta za jamii za afya na elimu wameweza kupiga hatua kwa kuweza kujenga shule 129 kati ya hizo shule 97 ni za Msingi na Sekondari ni 32 pia wanaendelea na ujenzi wa shule nyingine tisa katika ya shule hizo moja ni shule maalumu ya wavulama inayojengwa katika Manispaa ya Mpanda ,
Pia Mkoa uweza kujengewa na Serikali Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa ya kisasa ambayo imeisha anza kazi na fedha za ujenzi wa
awamu ya pili zimeisha fika na upande wa vifaa tiba wameandelea
kupata vifaa tiba vya kutosha ili kufanya hali ya wananchi kuendelea kuboleka
vilevile idadi ya magari ya wagonjwa yameongezeka kutoka 10 hadi
kufikia 16,
vIlevile kwa upande wa maji kumekuwa na ongezeko
kubwa na upatikanaji wa maji kwa sasa wapo asilimia 76.7 na
wanatarajia miradi inayoendelea kutekelezwa itakapo kuwa imekamilika
kutakuwepo na ongezeko kubwa la upatikanaji wa maji .
Mrimdoko amesema kulikowepo na migogoro ya muda mrefu ya ardhi ambayo wameweza kuitatua ambayo ameitaja baadhi kuwa ni mgogoro wa wananchi na jeshi la Wananchi , mgogoro wa Luhafwe ,Kashalami sitalike, Kua na Kabage
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Katavi Mwandisi Martin Mwakabende
amesema kwa nwaka wa fedha wa 2024/2025 wamepokea kiasi
cha shilingi Bilioni 15 kwa ajiri ya matengenezo ya barabara
Pia wamweza kupata fedha hivi karibuni kiasi
cha shilingi Bilioni 17 .6 kwa ajiri ya ujenzi wa madaraja matatu ya sitalike
Kibaoni na Mirumba na tayari wakandarasi wameanza kazi na wapo katika hatua
mbalimbali za ujenzi wa madaraja hayo .
Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe amempongeza
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa inayoifanya kwa kupitia
Mkoa wa Katavi ambao hapo awali ulikuwa nyuma lakini sasa hivi umekuwa ni
mkoa wa mfano kutokana na na maendeleo makubwa yalipo sasa kutokana
na fedha nyingi za maendeleo zilizoletwa .