RC KATAVI WALIOFAULU DARASA LA SABA WOTE KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA JANUARI.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumnza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Katavi ofisini kwake.

Na Walter Mguluchuma-Katavi

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua  Mrindoko  amewahakikishia Wananchi wa Mkoa wa Katavi  kuwa  wanafunzi wote  13, 887 walofaulu  mtihani  wa darasa la saba na kuchaguliwa   kujiunga na  kidato cha kwanza  mwaka 2025  katika shule mbalimbali zilizopo katika Mkoa wa Katavi.

Baadhi ya waandishi wa habari Mkoa wa Katavi,wakiwa katika kikao hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua  Mrindoko  amewahakikishia Wananchi wa Mkoa wa Katavi  kuwa  wanafunzi wote  13, 887 walofaulu  mtihani  wa darasa la saba na kuchaguliwa   kujiunga na  kidato cha kwanza  mwaka 2025  katika shule mbalimbali zilizopo katika Mkoa wa Katavi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko wakati alipokuwa  akitoa taarifa ya maandalizi  ya wanafunzi wanao jiunga na kidato cha kwanza.

Amewafahamisha wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwa  maandalizi ya mhula mpya wa masomo utakaonza January 13 Mwakani.

Amebainisha kuwa wanafunzi wote waliofanya mtihani wa kumaliza  darasa la saba  na  kuchaguliwa kujiunga na Sekondari  wanafunzi  wote  waliofaulu  wataanza masomo hapo mwakani baada ya kupangiwa wote  shule pasipo kuachwa mwanafunzi hata mmoja .

Amebainisha   kuwa katika wanafunzi hao wapo wanaokwenda kwenye shule za Kitaifa  na wengine wamepangiwa katika shule mbalimbali  zilizopo katika Mkoa huu  kwa hiyo wanafunzi wote waliochaguliwa wamepangiwa shule .

Mrindoko amesema Rais Dk Samia Suluhu Hassan ameleta fedhaambazo zimesaidia  kufanya maandalizi  ya kujenga  madarasa  mapya  311 wakati mahitaji ya Mkoa ilikuwa ni madarasa  283 kwa Mkoa mzima  hivyo kuna vyumba 28 vya ziada vya madarasa katika Mkoa huu.

 Kuhusu uandikishaji wa darasa la kwanza na awali  amesema  Mkoa huu umekuwa ukifanya vizuri katika uandikishaji  na mpaka sasa umefikia zaidi ya asilimia 34 ambayo bado ni asilimia ndogo hivyo amewahimiza wazazi wenye watoto waliofikisha umri wa kujiunga na darasa la awali  na la kwanza kuwapeleka watoto wao kujiandikisha .

Mrindoko amewaagiza viongozi wote wa Serikali kwenye maeneo yao kuhakikisha  watoto wote  wenye  umri wa kuanzia miaka minne wa fike kwenye shule za msingi kwa ajiri ya kuandikishwa  ili nao waweze kuanza masomo yao  mapema mwakani .

Amesisitiza kuwa  maelekezo ya Nkoa ni kuhakikisha kila wanafunzi anapata chakula cha  mchana shuleni  hivyo wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi   pamoja na walimu wakuu wasimamie ipasavyo ili wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waendelee kupata chakula  shuleni. 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages