Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda Joseph Lwamba akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari ofisini kwake. |
Na Paul Mathias-Mpanda
Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya
Mpanda Mkoa wa Katavi kimewaonya vikali baadhi ya wanachama wa CCM Wilaya ya
Mpanda kuanza viashria vya kuonyesha kutia nia za kugombea ubunge kwenye baadhi
ya Majimbo katika Wilaya ya Mpanda kabla ya wakati.
Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi kimewaonya vikali baadhi ya wanachama wa CCM Wilaya ya Mpanda kuanza viashria vya kuonyesha kutia nia za kugombea ubunge kwenye baadhi ya Majimbo katika Wilaya ya Mpanda kabla ya wakati.
Onyo hilolimetolewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda Joseph Lwamba mbele ya waandishi wa habari muda mchache baada ya kumalizika kwa kikao cha dhalula cha Kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya Wilaya ya Mpanda.
Lwamba ameeleza kuwa kumekuwa na
viasharia vinavyokinzana na maadili ya Chama kwa baadhi ya wanachama kuanza
kampeni za mapema zinazoonyesha nia ya kugombea nafasi za ubunge kwenye baadhi
ya majimbo katika wilaya ya Mpanda.
Ameeleza kuwa kamati ya siasa
imebaini mapungufu yanayoendelea kwenye chama hicho ambayo hayawezi kufumbiwa
macho huku kamati ya siasa ikielekeza baadhi ya mambo kufanyika kwa
walewalionza kuonyesha nia zao mapema za kugombea kabla ya wakati kufika.
Amesema kuwa kamati ya siasa
imeelekeza ni mwiko kutoa vifaa fedha au zawadi kwa viongozi na mwanachama
yeyote bila kufuata utaratibu kwa mujibu wa kanuni.
Amefafanua kuwa viomgozi wote
wakiwamo wabunge na madiwani waendelee kuchapa kazi za chama na chama
kinathamini mchango wao kwa kazi wanazoendelea kuzifanya.
Mwenyekiti huyo amesema zipo
taarifa rasmi na zisizo rasmi kwamba kuna watu wameanza kuzunguka majimboni kwenye
majimbo ya Mpanda Mjini na Jimbo la Nsimbo na wengine kwenye kata hali ambayo
inawafanya viongozi waliopo madarakani kushidwa kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Ameongeza kuwa viashiria hivyo wanachama wanaviona na wasio wanachama wanaviona huku akikisistiza kama chama hawata vumilia kuona hayo yakifanyika