Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumnza na waandishi wa Habari wakati akitoa salamu za Mwaka Mpya 2025 kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi mwananvua
mrindoko amewahakikishia wananachi wa Mkoa wa Katavi kwa mwaka wa 2025 kuwa
serikali ya Katika Mkoa wa Katavi itawatumikia wananchi kwa uadilifu katika
sekta zote.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi mwananvua mrindoko amewahakikishia wananachi wa Mkoa wa Katavi kwa mwaka wa 2025 kuwa serikali ya Katika Mkoa wa Katavi itawatumikia wananchi kwa uadilifu katika sekta zote.
Amebainisha hayo wakati akitoa
salamu za mwaka Mpya wa 2025 ofisini kwake kupitia waandishi wa habari ambapo
ameeleza kuwa serikali ya Mkoa wa Katavi na watendaji wake imejipanga vyema
kuwatumukia wananchi wa Mkoa wa Katavi kwa vitendo.
Mrindoko ameeleza kuwa kipaombele
cha kwanza kwa wanananchi wa Mkoa wa Katavi kuimarisha utoaji wa huduma
mbalimbali katika sekta zote ili wananchi hao waendelee kujivunia viongozi na
watendaji waliopo Mkoa wa Katavi.
‘’Jambo la kwanza ni kuimarisha
utoaji wa huduma kwa wananchi zilizopo katika sekta mbalimbali zikiwemo
afya,Elimu,Maji,na Barabara-Mrindoko’’
Ameeleza kuwa mkakati na msukumo
wa ndani ya Mkoa wa Katavi nikuhahakisha huduma hizo zinawanufaisha wananchi
kwa kiwango kikubwa na huduma hizo zikiwa bora zaidi.
Amesema kuwa fedha zitakazo letwa
na serikali zitasimiwa kwa uadirifu kwa
ili kutatua changamoto mbalimbali za wananchi kupitia miradi mabalimbali ya
maendeleo.
Kuhusu ukuzaji wa sekta ya
viwanda amesema kuwa ujio wa umeme wa gridi ya Taifa ambao kwa sasa umefikia % 76
unakwenda kuwa mkombozi wa kiuchumi katika sekta ya viwanda.
‘’Mkoa wetu ambalo lilikuwa
linaturudisha nyuma ni suala zima la upatikanaji wa huduma ya umeme kwaajili ya
uendeshaji wa viwanda ninayo furaha kuwa fahamisha kwamba mradi wetu wa umeme
wa gridi ya taifa umefikia % 76.-Mrindoko.
Ameeleza kuwa mkakati wa Mkoa wa
Katavi nikuhahakisha wanaendelea kutafuta wawekezaji wa kutosha katika sekta ya
viwanda kwakuwa tatizo la ukosefu wa umeme wa uhakika linakwenda kupatiwa
majawabu kupitia mradi wa umeme wa gridi ya Taifa.
‘’lengo letu ni kuipa msukumo hii
sekta ya viwanda kwa hali ya juu kwa sababu tayari tunayo matumaini kwamba
umeme wetu wa Gridi ya Taifa hauko mbali kufika ndani ya Mkoa wa Katavi-Mrindoko’’
Kupitia uwepo wa nishati ya
uhakika ya umeme amesema sekta ya kilimo , viwanda ,Madini,na ufugaji kwenye
Mkoa wa Katavi vitaenda kuimarika zaidi kwakuwa uhakika wa umeme utakuepo.
Ameeleza kuwa Halmashauri zote katika Mkoa wa Katavi kutakuwa na viwanda vya kutosha kulingana na mazingira ya Halmashauri husika ili kusisimua uchumi wa halimashauri hizo na wananchi kwa ujumla kupitia sekta ya viwanda.