Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akikabidhi zawadiya mwaka mpya kwa mkuu wa gereza la mahabusu la Mpanda zilizo tolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Na Walter Mguluchuma.
Katavi
Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Mahabusu la
Mpanda Mkoa wa Katavi wamefurahia kuanza mwaka wa 2025 kwa zawadi
waliopewa na Rais DKT Samia Suluhu
Hassan ikiwa ni sehemu ya salamu zake za mwaka mpya kwa makundi mbalimbali yenye
uhitaji .
Msaada huo wa kitoweo cha mbuzi wanne na vinywaji baridi umekabidhiwa
na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwananvua kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa mahabusu na
wafungwa wa Gereza hilo .
Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo Mkuu wa Mkoa Mwanamvua Mrindoko amesema ni vema wafungwa hao na mahabusu waendelee kuwa watu wema pindi wanapokuwa Gerezani na watakapokuwa wamemaliza vifungo vyao na kwenda kuishi kwenye jamii
Amesema pamoja na kukabidhi zawadi hizo pia anatumia nafasi hiyo kuweza
kuwafikishia salamu za Rais za kuwatakia heri ya mwaka mpya wafungwa wote na mahabusu wa Gereza hilo
Aidha Mrindoko
ameviagiza vyombo vyote vya Haki
jinai vihakikishe vinashirikiana katika
maswala ya undeshaji wa kesi
yazingatie sheria haki taratibu na kanuni zote na zile kazi ambazo haziitaji muda mrefu ziweze kusikilizwa mapema ziweze kumalizika kwa wakati .
Amelishukuru gereza la Mahabusu
la Mpanda kwa kazi kubwa wanayofanya ya
kutekeleza miradi mbalimbali
ambayo inawapa mafunzo wafungwa
ili wanapotoka waweze kwenda kuwa Raia wema kwenye Jamii,
Mkuu wa Mkoa wa Katavi akikabidhi zawadi kwa ajili ya gereza la mahabusu Mpanda
Ameomba mwaka wa 2025 uwe mwaka mwema kwa Mwenyezi MUNGU ajalie kwa kila mmoja haki iweze kutendeka kwake kwa maana ya wafungwa na mahabusu waliko kwenye gereza hilo na Askari Magereza waweze kushikwa mkono zaidi ili waendelea kuwalea vyema walioko kwenye gereza .
Nae Mkuu wa Gereza hilo Fred
Mwakatobe amesema anashukuru
sana kupokea msaada huo kwani kiukweli mahabusu na wamefurahi na wamefarijika na
wamejisikia ni sehemu ya jamii pamoja na kuwa wametengwa lakini wamejisikia
wapo kwenye jamii.
MWISHO